ETI YESU NI VALENTINE WAKO?? HIVI UNAJUA UNALOSEMA??
 |
| Picha ya aitwaye Valentine aliyekuwa |
Inakaribia February 14, huitwa siku ya Wapendano. Unaulizwa
maswali na watu, je, mtu aliyeokoka anaweza kushiriki Valentine day? Hili
kwangu linaweza kuwa swali gumu sana. Inawezekana wapo watumishi waliowahi
kujibu kwamba Wakristo hawapaswi kushiriki kwa sababu hii sio ya Kikristo,
kwangu inaweza kuwa ngumu kidogo kutumia kigezo kwamba sio ya Kikristo hivyo
watu wasijihusishe nayo.
Maana kama kigezo ni hicho tu kwamba sio ya Kikristo, swali
moja najiuliza; hapa Tanzania tuna sherehe za Muungano, Uhuru na Mapinduzi,
tuna zingine kama MEI MOSI, na zinginezo ikiwemo NYERERE DAY, sioni kama hizo
ni za Kikristo, lakini mbona wanashiriki?
Mimi nadhani kuna haja ya kurudi nyuma na kuchunguza
historia ya namna hii siku ilianzishwa, na nini malengo yake ya kuadhimishwa.
Mimi nilijipa muda huo tangu siku za nyuma, nimekuwa nikieleza maoni yangu sio
leo tu, na hapa nitaeleza tena kidogo.