Sunday, 14 February 2016


ETI YESU NI VALENTINE WAKO?? HIVI UNAJUA UNALOSEMA??


Picha ya aitwaye Valentine aliyekuwa
Inakaribia February 14, huitwa siku ya Wapendano. Unaulizwa maswali na watu, je, mtu aliyeokoka anaweza kushiriki Valentine day? Hili kwangu linaweza kuwa swali gumu sana. Inawezekana wapo watumishi waliowahi kujibu kwamba Wakristo hawapaswi kushiriki kwa sababu hii sio ya Kikristo, kwangu inaweza kuwa ngumu kidogo kutumia kigezo kwamba sio ya Kikristo hivyo watu wasijihusishe nayo.

Maana kama kigezo ni hicho tu kwamba sio ya Kikristo, swali moja najiuliza; hapa Tanzania tuna sherehe za Muungano, Uhuru na Mapinduzi, tuna zingine kama MEI MOSI, na zinginezo ikiwemo NYERERE DAY, sioni kama hizo ni za Kikristo, lakini mbona wanashiriki?
Mimi nadhani kuna haja ya kurudi nyuma na kuchunguza historia ya namna hii siku ilianzishwa, na nini malengo yake ya kuadhimishwa. Mimi nilijipa muda huo tangu siku za nyuma, nimekuwa nikieleza maoni yangu sio leo tu, na hapa nitaeleza tena kidogo.



 ASILI YA NENO VALENTINE

Neno Valentine linatokana na jina la jamaa mmoja wa Kikatoliki (leo tungesema alikuwa Padri) ambaye aliishi kwenye mji wa Roma huko Italy, alikuwa anaitwa VALENTINE au kwa Kiswahili Valentino. Aliishi enzi za utawala wa Claudius (Claudio).

 Nitakueleza ilikuwaje siku hii ikaitwa jina lake. Kuna dhana nyingi kuhusu siku hii, lakini ziko mbili zenye mashiko, kwangu mimi zote hazina uhusiano na UPENDO au UKRISTO bali mahaba au hisia za kimapenzi. Nitafafanua!

Katika kulifanya jeshi lake liwajibike katika vita, Mfalme Claudio aliwapiga marufuku Wanajeshi wake kuoa, lakini pamoja na marufuku hiyo huyu Padri Valentino aliendelea kufungisha ndoa za wanajeshi waliokuwa wanataka kuoa wakati mwingine pengine kwa siri.

 Jambo hili lilipogundulika kwa Mfalme Claudio Valentino alifungwa gerezani.
 Akiwa Gerezani huyu jamaa akajikuta anampenda binti mmoja wa Mfanyakazi wa gereza alilokuwa amefungwa. Nataka nisisitize hapa, kwamba alimpenda binti huyu ambaye hakuwa dada yake, wala mama yake, wala mpwa wake, wala mjukuu wake, wala uhusiano wowote wa damu, bali alimpenda KIMAHABA/HISIA ZA KIMAPENZI. Uzuri hapa ninyi wote ni watu wazima, mtakuwa mnanielewa ninachomaanisha!

Padri Valentine akifungisha ndoa ya askari
Kwa hiyo, upendo huu haukuwa wa kindugu/kirafiki ambao kwa Kigiriki tunaita (PHILEO) au haukuwa upendo wa Kimungu yaani AGAPE, au bali upendo wa KIMAHABA yaani EROS kwa Kigiriki, ambapo kwa Kiingereza tungesema romantic feelings. Huyu Padri alimtumia huyu binti kadi yenye maneno haya, NAKUPENDA, NI MIMI WAKO VALENTINO, neno nakupenda lililotumika hapa ni EROS na sio Phileo, Agape nk!

 Ifahamike pia kwamba wakati huo kulikuwa na siku kuu fulani ya kipagani ambayo iliadhimishwa kipagani, siku kuu hii iliitwa LUPERCALIA ambayo ilikuwa ikisheherekewa mnamo tarehe 15 februari. Lakini wasichojua wengi ni kwamba huyu LUPERCALIA alikuwa ni mungu wa kiroma, walimwamini katika masuala ya kilimo.
Baada ya Valentino kufa, siku hii ya LUPERCALIA mungu wa kipagano ikabadilishwa jina kwa heshima ya Valentino na kuitwa siku ya valentine au VALENTINE DAY. Hivi kweli Mkristo hujashtuka tu mpaka hapo?

 SWALI NA ANGALIZO
Kimazabau cha kufanya maombi kwa    
MtakatifuValentino
na sanamu yake
Je, kuna ubaya gani kwa Walokole kushiriki siku hii ikiwa mtu yuko na mkewe/mumewe na hawakuokotana vichochoroni? wamefunga ndoa ya heshima kanisani Je, upo ubaya kusheherekea katika hilo?

 Ndugu zangu kila kitu kina sababu zake katika ulimwengu wa roho
Ukiondoa hilo, leo hii kuna watu wanatumia Valentine Day kuwatumia mama zao, baba zao kadi nk, je, hii ndio asili yake? Kama sheria za ulimwengu wa roho zinafanya kazi, usalama wetu uko wapi mtoto wa kike anaposema baba yake mzazi ndiye Valentine wake? Au watu bila haya wanapoandika kwenye facebook eti Yesu ni Valentine wake?

 Nini kinaendelea kwenye ulimwengu wa roho? Sijakataza mtu, nimeweka maswali ambayo na mimi pia najiuliza, kama ni kujibu wote tusaidiane, lakini kumwita dada yangu wa tumbo moja au washirika wangu kanisani Valentine, duuh!! Inaleta KIGUGUMIZI hasa nikizingatia neno Upendo alilolitumia Valentine siku ile! NAWAPENDA!

(Andiko hili ni kwa msaada wa mtandao)
Mtakatifu Valentino wa Katoriki akipokea lozari
toka kwa Bikira Mariamu.




1 comment:

  1. Kweli mwalimu haistahili kwa mkristo kusherehekea hii siku.0756201989 & 0719386301.nitumie hata message mi ntakupigia nna shida na we mwalimu.ni Mimi Allan Joseph at Mganyizi

    ReplyDelete