Msalaba, ni moja ya kitu
aua alama ambayo niya maana sana katika maisha ya wakristo wengi, uwezi
kuongelea injiri pasipo kutaja msalaba ambao Bwana Yesu aliuwawa juu yake. Kwa
zaidi ya miaka elfu mbili sasa msalaba umekuwa na uhusiano mkubwa sana kanisa kwa
maana wakristo. Msalaba umekuwa kiwakilishi cha wokovu, ushindi, rehema,
tumaini pia umekuwa ishara ya Yesu Kristo na pia kanisa maana watu waonapo
msalaba umechorwa mahali popote ujua kuwa mahali hapo kuna mkristo au ukristo,
wakristo wametumia alama za misaraba katika makanisa, nyuma zao kuonyesha au
kukili mbele za watu juu ya Imani yao, wengine wamevaa shingoni na hata wengine
kuchora katika mavazi yao. Hakika msaraba umekuwa na uhusiano na muunganiko
mkubwa na maisha yetu pia na mwokozi wetu Yesu Kristo.
Lakini kabla ya Bwana Yesu kusurubiwa na kufufuka msalaba haukuwa na maana nzuri kwa mwanadamu yeyote kama leo hii, ulitisha na kuogopwa na wote na hakuna mtu ambaye alitaka kujihusisha nao kabisa.
Lakini kabla ya Bwana Yesu kusurubiwa na kufufuka msalaba haukuwa na maana nzuri kwa mwanadamu yeyote kama leo hii, ulitisha na kuogopwa na wote na hakuna mtu ambaye alitaka kujihusisha nao kabisa.
KIFAA CHA MATESO
Msaraba hapo zamani ulikuwa
ni kifaa kilichotumika kutesea watu kabla ya kufa, mtu alitundikwa msarabani
akiwa hai na kugongelewa misumari mitatu pekee kwenye viganja viwiri vya mikono
na miguu ukusanywa na kugongelewa pamoja, hakika yalikuwa mateso sana kwanza
ile misumari uliyogongelewa pia ni pale ukisimamwishwa maana mwili mzima ubebwa
na misumari mitatu mikubwa iliyokuwa mikononi na
miguuni, hakika ni maumivu makali sana.
miguuni, hakika ni maumivu makali sana.
KIFAA CHA KUAIBISHA
Msaraba ulitumika pia
kumwaibisha mtu, kila aliyetundikwa msarabani sharti alitundikwa akiwa uchi na
msaraba ulikuwa ukiwekwa maeneo yenye kusanyiko la watu na hasa katika milango
ya kuingilia mjini ili kufanya watu wote wanaoingia na kutoka mjini kuweza
kukuona wazi kitu ambacho ni aibu kubwa.
KIFAA CHA KUTISHA WATU
![]() |
Miili ya watu ikiwa imeachwa msarabani. |
KIHASHIRIA CHA LAANA
Biblia inakili kuwa kila
ambaye ametundikwa msarabani amelaaniwa na kwa sheria za wayahudi ambazo
walipewa na Mungu pia ni pale anapotokea mtu akatenda kosa la kustahili kifo
ambalo ni laana basi atundikwe msalabani ila usiku usifike mwili wake bado
ukiwa unaninginia msarabani bali ashushwe maana wasipofanya hivyo Mungu alisema
laana ya mtu huyo inakuwa juu ya nchi japo kwa warumi haikuwa hivyo wao mwili
wa mtu ulikaa hata zaidi ya siku moja ili kutoa fundisho na onyo kwa watu kuto
kutenda kosa kama alilotenda huyo aliyeuawa. Hivyo tunaona msaraba ulikuwa
ishara ya laana.
KIFAA CHA KIFO
Lakini zaidi ya yote
msaraba ulitumika kama kifaa cha kuulia mtu, watu ambao walihukumiwa kifi hasa
kifo cha aibu, maumivu na mateso basi msaraba ulikuwa ndiyo kazi yake kwa kuwa
mtu hakufa haraka bali alikuwa akifa kidogo kidogo ila kwa maumivu na uchungu
mkali sana, damu ilitulilika kidogo kidogo mpaka pale mwili ulipoishiwa na damu
na kushindwa kufanya kazi yake vizuri ndipo mtu ufa.
BWANA YESU NA MSARABA
![]() |
Msaraba, kimbilio la mataifa. |
Baada ya kupigwa sana
mijeredi thelathini kasolo mmoja na askari wa kirumi aliweza kupewa adhabu ya
kwanza ya kuubeba msaraba wake kwenda nao nje ya mji mahali paitwapo Goligotha
yaani fuvu la kichwa, aliubeba akiwa kachoka na mwenye maumivu makali sana na
kuanza kupita katika kinjia chembamba sana chenye kusheheni watu wengi wenye
kumsonga pande zote wengine wakimtukana, wengine wakimtupia mawe huku askari wa
kirumi wakimzingira kuhakikisha anafanikiwa kufikisha msaraba wake sehemu
husika na kweli alifanikia kufika na huko alikutana na waarifu wawili ambao nao
walihukumiwa kifo cha aibu na maumivu cha msaraba.
Hakika inasikitisha sana.
Akiwa Goligotha alivuliwa nguo na kuwa uchi kisha kugongelewa msarabani na
kusimamishwa na msaraba kutoka saa sita mchana mpaka saa tisa alasiri alipodai
kusikia kiu na akapewa siki yenye uchungu mkali, ndipo sasa akapaza sauti yake
akimwisema IMEKWISHAAA na akaitoa Roho yake ndipo nchi ilipotikisika na misingi
yake huku makaburi yakifunguka na miili mingi ya watu ikitokeza ndani yake na
kuingia mjini.
Baada ya siku tatu Bwana
Yesu yu hai, hakika yu hai milele.
MAANA MPYA YA MSARABA
Ukitaka kujua kuwa Yesu
Kristo alikuwa na nguvu ya ajabu ya kubadilisha uovu kuwa wema, giza kuwa nuru,
uzuni kuwa furaha, kilio kuwa kicheko, usiku kuwa asubuhi utaweza kuona kwanza
katika msaraba.
Msaraba hule hule ambao
ulikuwa ni kifaa cha kuaibisha, kutesa, kuua, kuuzunisha na ishara ya laana,
kifo n.k ameweza kuibadili kwa kifo chake na kufanya leo hii msaraba kuwa
ishara ya ukombozi, ushindi, tumaini, Amani n.k
Ni miaka elfu mbili sasa
tokea Mwokozi wetu Yesu Kristo kufa na kufufuka na kubadili maana ya msaraba.
Zamani ilikuwa ni mshangao kwa mtu kuvaa msaraba, kutundika msaraba katika
nyumba ya ibada, kuweka au kuchora msaraba nyumbani kwako au kwenye nguo maana
ni kifaa cha kuua, leo hii ni sawa ukute mtu kavaa shingoni kiti cha umeme, au
kachora picha ya kitanzi nyumbani kwake itashangaza maana ni vifaa vya kuua
lakini Bwana Yesu ameugeuza msaraba kutoka huko.
Msaraba leo unaimbwa kama
kimbilio la watu wenye kutafuta ukombozi, amani, tumaini, ushindi, mwongozo,
uponyaji n.k Lakini laity tukikumbuka kuwa msaraba ulikuwa ni kifaa cha kuua
hakika ni vigumu kukimbilia kitanzi, sumu, upanga, kiti cha umeme, bunduki kama
unatafuta tumaini, amani, furaha, wokovu maana haviwezi kufanya hivyo lakini
msaraba ulibadilishwa kutokana na nguvu ya kifo cha Yesu.
KILA MTU ANAO MSARABA
WAKE
![]() |
Askari wa Kirumi wakiwa wametundika miili ya watu kwenye misaraba pembezoni mwa njia. |
Msaraba ni shida, matatizo,
kama vile magonjwa, dhiki, umaskini, kukataliwa n.k Wengi tuna misaraba mingi
katika maisha. Misaraba ni vile vitu au mambo ambayo yanatupa mateso na aibu
mambo ambayo yanataka kutua yapo na unayo lakini Yesu anakuambia yabebe na
umfuate nayo.
Kama Bwana Yesu aliweza
kubadili msaraba wa aibu, mateso, uzuni na mauti kuwa tumaini, ukombozi,
ushindi basi anaweza kubadili na msaraba wako huo wa utasa, umaskini, ugonjwa,
talaka, kuachwa, kutoa kuolewa, kushindwa masomo, kukataliwa na ndugu na jamaa,
kufilisika na kufanya kuwa ushindi, furaha, kichekona tumaini hakika anaweza
kufanya na atafanya, alifanya kwa Ayubu mtu ambaye alizungukwa na misaraba
mingi kama kufiwa na watoto wote, kufilisika, kupoteza mashamba na mifugo na
kuumwa sana hakika Ayubu alibeba misaraba yake na kumfuata Mungu bila kukata
tamaa na mwisho kila ambacho alikuwa amepoteza aliweza kurudisha mara mbili
kitu ambacho labda hapo mwanzo hasingeweza lakini alipokubali kubeba misaraba
yake na kumfuata Mungu iliwezekana.
Hata Yusufu, alipatwa na
shida, taabu, kuonewa, kusingiziwa lakini aliweza kuibeba misaraba yake na
kumfuata Mungu, hakika hakumwacha Mungu na mwisho wa siku kuuzwa kwake utumwani
na ndugu zake kulikuwa ni njia ya kumpeleka Misri na kusingiziwa kwakwe na mke
wa bosi wake na kupelekwa gerezani kulikuwa ndiyo njia ya kumpeleka kwa mfalme.
KUBEBA MSARABA NI NINI?
Kubeba msaraba ni kule
kubaini shida na taabu ambazo unazo na kusimama imara zisije kuingilia Imani yako
kwa Mungu kwa namna yeyote na kukutenga na Mungu kwa hali yeyote. Kubeba
msaraba ni kule kuelewa hali uliyonayo na kusimama kwenye maombi kushindana
mpaka mwisho, ni kule kumwita Mungu ndani ya uzuni na kilio chako. Unapopatwa
na matatizo usiwaze kuwa utaangamia waza kuwa ni njia ya ukombozi, baraka na
ushindi. Matatizo uliyonayo siyo kipimo cha maisha yako, usitazame tatizo na
kusema sitaweza kuishi mda mrefu, usitazame tatizo na kusema nimekwisha au
kusema basi, tazama tatizo kama njia ya kuendea baraka, kumkaribia Mungu, kumjua
Mungu.
MATATIZO UJA ILI TUMJUWE
MUNGU
Tunaposoma Biblia
tunaweza kumjua Mungu alivyo na uwezo wake kutokana na matatizo waliyopata watu
wake kwa mfano “Mungu anaweza kuokoa” tukisoma kitabu cha Danieli tunaona jinsi
Danieli alivyotupwa katika shimo la simba lakini akataoka salama, pia juu
Shedraki, Meshaki na Abedinego walivyotupwa katika tanuru la moto na kutoka
hai, hakika tunajifunza Mungu anaokoa pia kwa wana wa Israeli walipokuwa Misri tunajifunza
Mungu anaweza kumtoa mtu kwenye utumwa, utumwa wa umaskini, magonjwa, mapepo
kama alivyowatoa utumwani kwa Farao n ahata alipojaribu kuwaangamiza aliweza
kuangamia yeye na jeshi lake.
Ukubwa wa Mungu tunaujua
tunaposoma kuwa aligawa bahari, alisimamisha jua wakati wa vita, alishusha mawe
wakati Israeli ikipigana na adui zao na mengine mengi.
Hivyo misaraba uliyonayo
pia ni darasa ambalo Mungu anataka ujifunze kuhusu yeye, usikubali msaraba
ulionao kuwa ishara ya kifo, aibu, uzuni kwako bali simama imara na Mungu
ataugeuza kuwa amani, ushindi na furaha.
Mwl. Judicate Fredy
0765544589
0623655889
No comments:
Post a Comment