Saturday, 10 September 2016

JINSI YA KUTUNZA NDOTO YAKO ILI IWEZE KUTIMIA


Tunaposoma Biblia tunaona Mungu mara nyingi akisema na watu kupitia ndoto wawapo wamelala kama vile Ibrahimu, Yakobo, Yusufu, Suleimani, Yusufu (baba wa Yesu), Petro n.k  Na bado mpaka leo Mungu anaendelea kusema na watu kupitia ndoto lakini baadhi ya watu upuuza ndoto kwa kkuto kujua ndoto ni kitu gani katika maisha ya kiroho.
Kimsingi ndoto ni picha za matukio

1. KUSHIKA SHERIA ZA MUNGU

Sheria za Mungu ni Neno lake, ili uweze kutunza ndoto yako na kuifanya itimie sawa na Mungu alivyopanga na wakati usika ni vizuri kusoma Neno la Mungu na kulitimiza kama lisemavyo. Unapoona umeenda nje ya Neno la Mungu na kutenda dhambi geuka mara moja na utubu na kumwomba Mungu akaupe nguvu za kushika sharia yake na songambele.

Ndoto ni kama mshumaa uwakao, unahitaji kutunzwa usije
kuzimwa na upepo uvumao wa adui Shetani na wakala wake.
2. KUISHI MAISHA YA MAOMBI

Watu wengine kwa kuwa wanajua ndoto ni bayana na hakika zitokee hivyo wakiota tu ndoto uacha kuomba na kusema zitatokea bila kujua maombi pia uhitajika kutengeneza njia ya kuelekea kwenye ndoto yako kwa mda usika. Lazima kama mkristo kishi maisha ya kushindana na kujua wakati wote kunapotokea jambo la kimungu basi Shetani naye ujiinua hivyo unapoota ndoto njema ya kimungu tambua Shetani naye anajiandaa kuzuia isitokee hivyo kaa katika maombi daima mpaka iweze kutimia.


3. KUWA MWAMINIFU KATIKA KUMTOLEA MUNGU.

Kumtolea Mungu siyo ombi bali ni sheria na kanuni moja wapo ya msingi kwa kila mtu wa Mungu,  katika kumtolea Mungu kuna baraka, lakini kwa hasiyemtolea kuna laana hivyo ni vizuri kutambua utoaji wa sadaka kama fungu la kumi (zaka) na sadaka nyengine ni muhimu sana. Mungu alisema katika kitabu cha Malaki kuwa unapomtolea Zaka yeye atakemea yule alaye, anaposema yule alaye anamaanisha kuna mashetani ambao uweza kutengeneza matukio au vitu ilikutafuna mapato yako kama vile magonjwa, majanga, kesi na mengine mengi, unakuta mtu Mungu amekuonyesha katika ndoto utapata cheo fulani kazini na unapokalibia kupata kwa kuwa haukuwa mwaminifu na sharia ya Mungu inasema lazima umtolee sadaka na unakuta wewe haumtolei hivyo yeye alaye anakuja kwa mfano wa kesi ya uongo kazini na unaonekana kuna fedha uliiba na watu wanaanza kuamini ni kweli na kumbe siyo na kukuta unakosa uaminifu kwa bosi na anaacha kukupandisha ngazi na unabaki pale pale na kushangaa na kuanza kuona mbona uliota unapanda na haujapanda kumbe ni kule kuto kumtolea Mungu.

4. KUWA MWAMINIFU KWA MUNGU KATIKA KAZI ZAKE
Ni vizuri kuwa mwaminifu katika kazi zake, kazi za Mungu ni nyingi siyo kuhubiri au kuimba bali hata kushuhudia watu Neno la Mungu, kuwaombea watu wanapopatwa na shida kwawao kujua au kuto kujua, kusaidia watu wenye uhitaji, kufanya usafi kanisani, kualika watu wa kazini, mtaani au sehemu mbalimbali kanisani n.k Kazi za Mungu ni shughuli zote au vitu vyote ambavyo ukifanya vinamrudishia Mungu utukufu na heshima na unapokuwa mwaminifu kwa maana ya kujitoa na kujituma, kufanya kwa kumaanisha siyo kwa unyonge au kulazimishwa na mtu, kuto kuona aibu ufanyapo n.k Kwa kufanya hivi unamfanya Mungu kujishugulisha na mambo yako na kukufanikisha.

5.  KUISHI VIZURI NA WATU

Mungu usaidia watu, ubariki watu, uponya watu n.k lakini kupitia watu. Mungu anapotaka kumbariki mtu utumia watu, Mungu hawezi kukushushia fedha chumbani kwako ila anaweza kukupatia wazo na kuanza biashara na katika biashara akakuletea watu ambao wakanunua bizaa zako na kuziongelea vizuri na kukuletea fedha ambazo zikawa baraka hivyo ni vizuri kuwatendea watu vizuri kwa kuwa hao hao utumiwa na Mungu siku ya mwisho, kama utaishi nao vibaya itakapofika wakati wa watu kutumiwa ili kufanikisha ndoto yako watu hao watakuwa hawawezi kutumiwa maana wameumizwa na wewe kwa kuwatukana, kuwasema vibaya, kuwadharau n.k hivyo hawataweza kukujia, unapoishi na ndugu au jirani vizuri ni rahiisi Mungu kusema nao juu ya wewe na wakakusaidia. Jambo jengine ni kuwa Mungu anapenda watu sana na ukitaka kujua kiwango cha upendo wake ni kule kujifanya mwanadamu na kufa msalabani kwaajili yao, hivyo unapoishi vizuri na watu na kuwasaidia unampendezesha Mungu maana wanadamu anawapenda sana na unapojihusisha na watu wake nay eye anajihusisha na wewe.

6.  KUWA MSIRI
Unapoota ndoto au kuwa na ndoto kila mtu siyo wa kumwambia ndoto yako maana wengine ni adui, tunaona Yusufu aliwaambia ndugu zake na hao hao wakata kumuua kwa kumwonea wivu juu ya ndoto zake, ni vizuri unapoota ndoto au kuwa na ndoto usimwambie kila mtu, kuwa makini maana siyo kila ndoto ya watu kujua maana ndoto nyingine niza wewe pekee kujua na siyo wengine. Kabla ya kumshirikisha mtu ndoto yako, jiulize je Mungu ameniruhusu kuwaambia watu na ukijua hajakuruhusu au kukuambia acha mara moja usije kuwaambia watu wakaanza kushindana na ndoto zako au kufanya vita na wewe kwa wazi au sirini na mwisho kuichelewesha ndoto yako. Kutunza siri pia ni moja ya sifa ya Mungu na watu wa Mungu pia.


Kama mkristo ni vizuri kuyajua haya na kufanyia kazi ili kuishi na kufika pale Mungu ametaka ufike.

No comments:

Post a Comment