Sunday, 24 July 2016

JINSI YA KUKUZA UHUSIANO WAKO NA ROHO MTAKATIFU (SEHEMU YA 2)


Waandishi wa Agano jipya kamwe hawakusitasita kuheshimu na kuiinua nafsi ya tatu ya utatu mtakatifu (trinity), na wamekuwa wakirudia kusisitiza umuhimu wa kuishi ukiwa na uhusiano naye. Kasehemu moja, Yesu anawaambia wanafunzi wake kuwa ni kwa ajili yao na faida yao kuwa yeye awaache na kurudi mbinguni ili kwamba aweze kuwatumia Roho Mtakatifu (Taz Yohana 16:7). Hakika hii gharama na kujitoa kwa ajabu kwa umuhimu wa huduma ya Roho! Yesu kwa kusema hivyo alikuwa akimaanisha kwamba ni bora kuwa na Roho Mtakatifu  kuliko kuwa na mwana wa Mungu katika mwili (personal)! Yesu alibidi kuondoka ili Roho Mtakatifu aweze kuja, kwa maneno mengine tena ni kuwa ilibidi Yesu kujitenga na wanafunzi wake mwilini ili Roho Mtakatifu aje, kuwa na Yesu mwili siyo bora kuliko kuwa na Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu anahitaji kuwa karibu na wewe katika maisha
yako.
Mitume wa Yesu walikuwa na Yesu kwa takribani miaka mitatu, wakimsikiliza mafundisho yake, na kujifunza katika mifano yake, lakini haikutosha. Yesu aliwaambia rafiki zake (wanafunzi wake) kuwa hawakuwa bado kumtumikia yeye mpaka pale watakapopokea nguvu ya Roho Mtakatifu (Tazama Luka 24:49). Kama Roho Mtakatifu ni wamuhimu hivyo kwa Yesu na mitume, hivyo niwamuhimu kwetu pia.

Nina amini kuwa hakuna ukweli sahihi kwa wakristo leo zaidi ya ukweli wa Roho Mtakatifu. Hebu sikiliza baadhi ya watu wakubwa wa Mungu, ambao ni wainjilisti na wahubiri waliowahi kutokea duniani wakielezea faida za Roho Mtakatifu. Jack Hsayford, Mchungaji kiongozi wa kanisa la The Way in Van Nuys, mjini California Marekani, akielezea mtazamo wake juu ya Roho Mtakatifu, aliweza kueleza faida za Roho Mtakatifu hivi:
Roho Mtakatifu siyo nguvu ya kujiunganisha na kupokea
utakacho ila anahitaji uhusiano na wewe pia.

Ni Roho Mtakatifu ambaye ulipa uhai Neno, Ndiye uleta uwepo wa kimungu kwangu...
Ni Roho Mtakatifu ambaye utia nguvu maombi na sifa 
Ni Roho Mtakatifu ambaye unifundisha na kuniongoza maisha matakatifu ili Kristo aonekane ndani yangu na ulimwengu umwone.
Ni Roho Mtakatifu ambaye uleta karama na vipawa ndani yetu na kuwa na huduma na kuweza kumtumikia Mungu kwa viwango atakavyo.
Ni Roho Mtakatifu ambaye anayeleta upendo, neema na roho ya umoja katika moyo wangu; hivyo siyo kwamba nawapenda waliopotea na kupenda kuwaona wanakuja kwa kristo, lakini nawapenda wakristo wote, na kukataa kuwa chombo cha kuumiza mwili wa kristo - kanisa.

Lakini rais wa Crusade for Christ na muhubiri Bill Bright ameandika kuhusu huduma ya Roho Mtakatifu katika moja ya kitabu chake akisema:

Roho Mtakatifu utuongoza (Yohana 1:13), Ututia nguvu (Mika 3:8) na utufanya watakatifu (Warumi 15:16). Ubeba ushuhuda katika maisha yatu (Warumi 8:16), utufariji (Yohana 14:16-26) na utupatia furaha (Warumi 14:17).....

Kama mwalimu wetu wa kweli wa kiroho, Roho Mtakatifu uangazia nia zetu kwa kutuangazia nia ya Kristo (1 Wakorintho 2:12-13) na kutufichulia mambo ya Mungu ya sirini (Isaya 40:13-14)....
Roho Mtakatifu akishukia mitume kwa umbo moto na
hua siku ya Pentekoste.

Unapokuwa umejazwa Roho Mtakatifu, Biblia inakuwa hai, maombi unayoomba yanakuwa muhimu sana, ushuhuda wako unakuwa wenye mguso wa hali ya juu na utii. Na matokeo ya utii wako katika maeneo hayo ni kukuwa kwa imani yako na kuwa mwenye kukuwa katika maisha yako ya kiroho. Watu wengi uomba kwa mazoea na bila utaratibu lakini unapokuwa na Roho Mtakatifu unakuwa hauombi kwa mazoea ila unaomba kwa makusudi hivyo ufanya maombi yako kuwa ya muhimu maana yanaombwa kwa wakati yakiongozwa na Roho Mtakatifu na yenye mguso na utii wa neno la Mungu na mapenzi yake.

Haijarishi Theolojia inasema nini au inatafsiri vipi, lakini wanaume na wanawake wa Mungu ukubaliana kuwa Roho Mtakatifu ni ufunguo wa maisha halisi ya kikristo. Nina amini ni sahihi kusema hivi:

Haijarishi ni kiwango gani unajua Biblia,
Haijarishi ni kiwango gani unajuwa kujisimamia na kujiongoza,
Haijarishi ni kwa jitihada gani umejaribu kumtumikia kwa kiwango fulani na kumpendeza Mungu,
Kama hauna uhusiano na ukaribu naRoho Mtakatifu katika maisha yako ya ukristo hayajafanya kazi kwa sababu maisha ya mkristo siyo mfundisho fulani kwamba unafundishwa kisha unashika na kuwa mkristo ila ukristo ni uhusiano wa Mungu kupitia Roho Mtakatifu na Yesu Kristo. Kama hauna uhusiano na Roho Mtakatifu ni ngumu kuwa na uhusiano na Mungu na kama hauna uhusiano na Mungu wewe siyo mkristo maana ukristo ni uhusiano na Mungu.

Kusudi la kuandika mfululizo wa somo hili ni kukusaidia kuingia katika uhusiano muhimu na Roho Mtakatifu ili uweze kupata uzoefu katika namna kubwa na kuwa rasilimali ya Mungu ili Mungu kukutumia  kwa viwango vya juu.

UHUSIANO NA ROHO MTAKATIFU

Wakristo wengi wanakuwa na wakati mgumu sana kuhusu Roho Mtakatifu kutokana na kushindwa kufahamu Roho Mtakatifu ni nani. Ufikiri Roho Mtakatifu ni nguvu fulani hivi ya kimungu, wengine uzani Roho Mtakatifu ni Switch ya umeme au ni umeme ambapo mtu uenda na kuchomeka waya ili kuvuta umeme uingie kwenye kifaa chake kifanye kazi hivyo uende kujiunganisha kwa Roho Mtakatifu ili kupokea kile wanachotaka. Lakini uwezi kuwa na uhusiano na nguvu (force) hata chanzo cha nguvu (source of power). Ila unaweza kuongoza na kutawala nguvu au chanzo cha nguvu kwa kuwasha na kuzima lakini uwezi kuwa na uhusiano na "Power Supply", jenereta hata umeme wenyewe ila unaweza kuwa na uhusiano wa kweli na wenye upendo na nafsi na utashi na ndiyo maana unaweza kuwa na uhusiano na mwanadamu maana anayo nafsi na utashi. Hivyo kama tunasema tunatakiwa kuwa na uhusiano na Roho Mtakatifu basi tunatakiwa kuhama kuwaza kuwa Roho Mtakatifu ni nguvu fulani au chanzo cha nguzu za kimungu bari anayo sifa ya nafsi na utashi kama mtu.

ROHO MTAKATIFU NI UTU (Holy Spirit is the Person)

Tuna maana gani tunaposema Roho Mtakatifu ni utu (person)? Kwanza kabisa hatumaanishi Roho Mtakatifu kuwa anao mwili (physical body), hapana, kwani kuwa na mwili siyo kinachofanya wewe uwe mtu maana hata unapokufa na roho yako ikiachana na mwili wewe bado ni "mtu" ndiyo maana katika kitabu cha Ufunuo 20:15 inasema "Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto" tunajua ndiko hili linaongelea baada ya watu wote kufa na kufufuliwa siku ya mwisho na kusimama mbele ya Yesu katika hukumu, tunajua watu hao ni roho lakini Biblia inawaita watu kwa maana kinachofanya mtu kuwa mtu siyo mwili ila nafsi yenye utashi. HIvyo tunaposema Roho Mtakatifu ni mtu au anao utu hatuna maana ni mwanadamu au anao mwili wa mtu, hapana, ila anao utashi wake, nia na mengine.
Roho Mtakatifu anaitaji uhusiano na wewe, uhusiano kama mtu na rafikie

Don Stewart, katika kitabu chake kiitwacho "95 Questions People Ask About the Holy Sprity" (Maswali 95 watu wanayouliza kuhusu Roho Mtakatifu) ameeleza juu ya utu wa Roho Mtakatifu kwa kufafanua namna nne ambazo Roho Mtakatifu anaonekana ni utu:

1. Roho Mtakatifu anazo tabia ambazo mtu anazo.

Yeye ni mwenye kufikilia
Yeye anaakili (1 Wakorintho 2:10-11)
Anazo hisia tena hisia za mndani (Torati 15:30, Waebrania 10:29)
Anauwezo wa kuchagua na kufanya maamuzi (Yohana 16:7)
Anaomba (Waebrani 8:26)
Hakika vitu hivi nguvu haiwezi kufanya au chanzo cha nguvu ila ni chenye utu tu ndiyo kinaweza kuwaza, kuwa na hisia, kufanya uchaguzi na maamuzi na pia kuomba na kule kusema kuomba ni kuwa na mapenzi yake binafsi hivyo unaposema mapenzi binafsi neno binafsi linatokana na neno nafsi na nafsi uwepo kwenye kitu chenye utashi ambacho ni utu hivyo Roho Mtakatifu siyo nguvu, upako au chanzo cha nguvu maana anayo nafsi.

2. Roho Mtakatifu anavitendo kama mtu.
Anafanya vitu ambavyo mtu anaweza kufanya kama:
Anaweza kufundisha (Yohana 14:26)
Anaweza kuzungumza (Wagalatia 4:6)
Anaweza kufariji (Yohana 16:7)
Anaomba (Warumi 8:26)
Hakika nguvu haiwezi kufundisha, kuzungumza, kufariji na kuomba ni chenye utu tu kinachoweza kufanya haya.

3. Roho Mtakatifu utendewa kama mtu.
Anaweza kutaka kudanganywa (Matendo 5:3)
Anaweza kuwa mwenye uzuni/kuhuzunishwa (Waefeso 4:30)
Anaweza hasiheshimiwe (Matendo 7:51)

Mahali popote katika historia tukitazama Roho Mtakatifu ametendewa kama mtu na ametenda kama mtu siyo kama nguvu mfano ameitwa, ameombwa, amekaribishwa, ametukuzwa, amesubuliwa, amepokewa na mengi hivyo Biblia nzima ametendewa kama nafsi yenye utu na siyo nguvu fulani.

Lakini mwisho kabisa Roho Mtakatifu ni mmoja kati ya utatu mtakatifu (trinity), uelezewa kuwa ni mwenye usawa wa utu katika utatu mtakatifu (Taz Mathayo 28:19, 2 Wakorintho 13:14). Anashiriki uhusiano mtakatifu na uliotukuka na Mungu Baba na Yesu Kristo mwana Mungu milele yote.

*********************     ITAENDELEA SEHEMU YA TATU             *********************

Kama una swali, maoni au ushauri unaweza kuwasiliana nami Mwalimu Judicate:
Simu: 0765 544 589 au 0623 655 889
Barua pepe: judicatemnyone@gmail.com




No comments:

Post a Comment