: Mwana wa Mungu lazima uvuke hapa!
(Chakula, Vinywaji, Mavazi na kesho)
Mathayo 6:25-34
25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
KWANINI NIMEAMUA KUZUNGUMZIA MAMBO HAYA MANNE?
1. Siyo standard ya wana wa Mungu Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta kwa lugha rahisi kuhangaikia Chakula, Vinywaji, Mavazi na kesho ni maisha ya chini kabisa.
2. Mungu ana mpango bora Zaidi, utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa
3. Mungu anashangaa, kwa nini tunahisi kwamba ni kazi yetu kufanya haya kama vile haimhusu wakati anafanya vizuri kabisa kwa ndege na maua Hatazidi sana kuwavika ninyi
4. Kutomwamini Mungu katika haya ni uhaba wa Imani kitu amabacho lazima kishughulikiwe kwa kuongeza wingi wa Imani. Mungu anasema hatumwamini. Wakati yeye anasema 1 Petro 5:7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. Kama anajishughulisha sana na mambo yetu na sisi tunajitutumua kana kwamba amelala.
Kumbuka: Mwenye Haki ataishi kwa IMANI (Habakuki 2:4, Warumi 1:17, Galatia 3:11, Ebrania 10:38)
5. Kujisumbua/kujitesa kwa mawazo ya kupata vitu hivyo huwa haileti majibu. Worrying or being anxious about them doesn’t change anything.
6. Kutesekea kesho ambayo hujaifika ni ubatili, ni vyema kuishi leo kwa ukamilifu wake. Mungu ameweka utaratibu wa kesho kujitengeneza kama leo itajitosheleza. Sisi hatukuumbwa kwa ajili ya siku, ila siku iliumbwa kwa ajili yetu. Je, nani mtumishi wa mwingine? Siku au wewe?
7. Mungu kwenye utaratibu wake anajua tunayahitaji haya mambo. Na yapo kwa ajili yetu..
Unaweza ukawa unajiuliza, aaah sasa tufanye nini?
KUMBUKA HILI SIKU ZOTE: MUNGU ANATAKA TUJUE KUWEKA VIPAUMBELE…
1. Kipi kinaanza na kipi kinafuata?
2. Nikifanya kipi ili nipate nyingine? Multiplier-effect.../ Cause-Effect Model
Ni sawa na Mungu kusema kuna mambo ukifanya, HUTAHANGAIKA TENA JUU YA *Chakula, Vinywaji, Mavazi na kesho
UFALME WA MUNGU NI ZAIDI YA HAYO *Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu*Warumi 14:17
KWA HIYO, UKIAMBIWA TAFUTA UFALME UNATAFUTA NINI? Haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu
Anayesumbuka haishi kama mwenye haki, hana Amani, wala hana furaha………
MATAIFA =WATU WASIOMJUA MUNGU hawana components hizo (haki na amani na furaha) kwani hawana Roho Mtakatifu.
WEWE AMBAYE UMEOKOKA UMEJAZWA ROHO MTAKATIFU, TAFUTA UFALME WA MUNGU SIKU ZOTE (haki na amani na furaha)
JE, UNAPATA AMANI JUU YA MAMBO UNAYOYAFANYA?
JE, UNAPATA FURAHA?
JE, UKO KWENYE HAKI YA MUNGU?
Haki na amani na furaha huwezi kutenganisha, ukipoteza moja, umepoteza vyote na utakuwa umeacha kuishi kifalme!.
KATIKA JINA LA YESU, KUTOKA KUSUMBUKIA VYAKULA, MAVAZI, VINYWAJI NA KESHO AMBAZO ZINALETA STRESS, MUNGU AKUPE KUISHI MAISHA YA JUU AMBAYO MAHITAJI YAKO NI KAMA MKATE WA KILA SIKU KWANI UFALME WAKE UMEKUJA KWANZA. UFALME WA MUNGU UKIJA SIWEZI KUHANGAIKIA MKATE WANGU WA KILA SIKU WALA KUTAHAYARI KWA AJILI YA KESHO, MIMI NI ZAIDI YA NDEGE, MIMI NI ZAIDI YA MAUA YA KONDENI. SIKU ZIMEUMBWA ILI KUFANIKISHA MAMBO YANGU NA SIYO MIMI KUTESEKEA, NITATAFUTA AMANI, FURAHA NA HAKI….
….AMEN….
Mwl. Judicate Fredy
No comments:
Post a Comment