Tunaposoma Biblia tunaona Mungu
mara nyingi akisema na watu kupitia ndoto wawapo wamelala kama vile Ibrahimu,
Yakobo, Yusufu, Suleimani, Yusufu (baba wa Yesu), Petro n.k Na bado mpaka leo Mungu anaendelea kusema na
watu kupitia ndoto lakini baadhi ya watu upuuza ndoto kwa kkuto kujua ndoto ni
kitu gani katika maisha ya kiroho.
Kimsingi ndoto ni picha za matukio
1. KUSHIKA SHERIA ZA MUNGU
Sheria za Mungu
ni Neno lake, ili uweze kutunza ndoto yako na kuifanya itimie sawa na Mungu
alivyopanga na wakati usika ni vizuri kusoma Neno la Mungu na kulitimiza kama
lisemavyo. Unapoona umeenda nje ya Neno la Mungu na kutenda dhambi geuka mara
moja na utubu na kumwomba Mungu akaupe nguvu za kushika sharia yake na
songambele.
 |
Ndoto ni kama mshumaa uwakao, unahitaji kutunzwa usije kuzimwa na upepo uvumao wa adui Shetani na wakala wake. |
2. KUISHI MAISHA YA MAOMBI
Watu wengine kwa
kuwa wanajua ndoto ni bayana na hakika zitokee hivyo wakiota tu ndoto uacha
kuomba na kusema zitatokea bila kujua maombi pia uhitajika kutengeneza njia ya
kuelekea kwenye ndoto yako kwa mda usika. Lazima kama mkristo kishi maisha ya
kushindana na kujua wakati wote kunapotokea jambo la kimungu basi Shetani naye
ujiinua hivyo unapoota ndoto njema ya kimungu tambua Shetani naye anajiandaa
kuzuia isitokee hivyo kaa katika maombi daima mpaka iweze kutimia.