![]() |
| Roho Mtakatifu yupo kwa watu wote wa mataifa walio mwamini Bwana Yesu na kumpa maisha yao. |
la plastiki ambalo ndani yake kulikuwa na cheni za dhahabu na pete zenye almasi ambazo zen
ye thamani sawa na dola zaidi ya 22000, jambo hili liliweza kushangaza watu kuwa iliwezekana
je mzee yule kuishi maisha yale muda wote na kufa na njaa akiwa mwenye fedha na mali zote hizo?!!! Tukio hili lilipamba magazeti na televisheni mbalimbali kama tukio la ajabu, polisi walipofanya uchunguzi waligundua kuwa mali zile zilikuwa zake na mjini New York alikuwa na nyumba nzuri, hakika hili ni jambo la kushangaza.
KUAMUWA KUFANYA MAISHA YA KIKRISTO "KUFANYA KAZI"
Mzee huyu ni picha halisi ya kanisa leo. Mungu amembariki kila mkristo kwa rasilimali za ajabu. Ametuumba na kutufanya kuwa Wafalme na Makuhani (tazama Ufunuo 1:6). Ametupatia baraka zote za rohoni (tazama Waefeso 1:3), na ametupatia mamlaka juu ya majeshi yote ya adui zetu (tazama Luka 10:19). Amefanya nguvu zake mwenyewe zisizo na mipaka (omnipotent power) kupatikana ndani yetu (tazama Waefeso 1:19-20).
Biblia inatuongoza katika vitu hivi alivyotupatia Mungu na jinsi gani Mungu amekusudia tuzitumie. Katika Yohana 14:12, Yesu ametuahidi kuwa kama tutamwamini, tunaweza siyo tu kufanya yale aliyofanya yeye ila na zaidi ya yake aliyofanya yeye. Katika barua yake kwa Waefeso, Mtume Paulo anasema nguvu iliyondani yetu ni kama nguvu ambayo ilimfufua Yesu siku ile ya tatu kutoka kaburini (Waefeso 1:19-20). Nguvu hii inatuwezesha kupeleka injili ulimwenguni mwote (tazama Matendo 1:8), na uona watu wakikombolewa kutoka katika nguvu za giza na kuingizwa katika Ufalme wa Mungu.
![]() |
| Mungu amekwisha kutubariki baraka zote za rohoni. (Waef 1:3) |
Wakristo wengi, hata hivyo, hawaelewi kitu hicho ambacho Mungu ametupatia. Wengi wanaishi katika umaskini wa kiroho, wanaishi kama viumbe wa kawaida tu na kumbe sisi si wakawaida, sisi ni viumbe watofauti ni "washirika wa tabia ya Uungu" maana imeandikwa "Tena kwa hayo ametukirimia (ametupa) ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washiriki wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa" hiyo ni (2 Petro 1:4), lakini tunajikuta tunajifanya watu wa mwilini (1 Wakorintho 3:3).
Mkristo wa wiki kwa wiki, kuudhulia ibada kanisani, kusoma masomo ya Bibli (Bible studies/Theology/Divinity), kushika desturi fulani ambazo tumeambiwa ni muhimukwa maisha ya mkristo mzuri ila ni michezo ya kidini tu. Lakini hatuoni ushuhuda wa ukristo wa Agano Jipya. Hii inatusababishia kushindwa kuwa na nguvu ya kustahimili majaribu na vitisho katika maisha yetu ya kila siku, na tukitikiswa kidogo na ulimwengu tunaumia sana.
UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU
Hakika inashangaza kuona wastani mdogo wa wakristo ambao wanajua kuhusu Roho Mtakatifu, Wakristo wengi wanaweza kukuambia kitu kuhusu Yesu, wengine kukuelezea na kukupa wazo zuri kuhusu Mungu Baba, lakini linapokuja swala la Roho Mtakatifu, wanakosa maneno ya kusema.
![]() |
| Biblia ina maneno mengi ya kusema kuhusu Roho Mtakatifu |
Lakini bado Biblia ina maneno mengi ya kusema kuhusu Roho Mtakatifu. Sura ya kwanza ya kitabu cha Mwanzo tuna mwona Roho Mtakatifu akiwa ameshuka na kutulia katika vilindi vya maji duniani na kila Mungu Baba alichotamka Roho Mtakatifu alikifanya hii kuonyesha Roho Mtakati alikuwa wa muhimu sana kati uumbaji maana alifanya vyote vilivyo tamkika kutokea (Mwanzo 1:2) pia katika kitabu cha mwisho katika Biblia, kitabu cha Ufunuo sura ya mwisho tunamwona Roho Mtakatifu akiungana na bibi harusi wa (Kanisa) kuomba juu ya ujio wa pili wa Yesu Kristo. Kupitia Neno tunaona Roho Mtakatifu ameshiliki ipasavyo katika kazi za Mungu duniani.
Lakini kwa nini wakristo wengi hawana uhakika kuhusu Roho Mtakatifu? Wakristo wengine wamefundishwa kuwa siyo sawa kuchunguza au kumwongelea Roho Mtakatifu. Utawasikia wakisema "Sitaki kuongelea kuhusu Roho Mtakatifu. Ila nataka kuongelea kuhusu Yesu". Kwa maneno hayo jambo hili linawezekana kuonekana la kiroho, lakini siyo jambo la kibibla hata kidogo.
Yesu alitangaza adharani kuwa moja malengo ya huduma yake ni kuleta watu katika nguvu (dynamic power), Maisha ya kujitoa ya kuwa na uhusiano na Roho Mtakatifu.
"Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na neon hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadae; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa."
(Yohana 7:38-39)
Yohana mbatizaji alitabiri juu ya Yesu kusema:
"Yohana alijibu akawaambia wote, kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.."
(Luka 3:16)
![]() |
| "yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.." |
Roho Mtakatifu alikuwa maarufu sana katika ujumbe wa mitume waliokuwa wakisambaza ulimwenguni kote. Katika siku ya Pentekoste, mtume Petro alitangaza kwa maelfu kwamba wale walio amini katika Yesu watapokea zawadi ya Roho Mtakatifu:
"Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu"
(Matendo 2:38)
...............................................ITAENDELEA SEHEMU YA PILI..................................




amen pastor
ReplyDelete