Friday, 14 October 2016

MSARABA



Msalaba, ni moja ya kitu aua alama ambayo niya maana sana katika maisha ya wakristo wengi, uwezi kuongelea injiri pasipo kutaja msalaba ambao Bwana Yesu aliuwawa juu yake. Kwa zaidi ya miaka elfu mbili sasa msalaba umekuwa na uhusiano mkubwa sana kanisa kwa maana wakristo. Msalaba umekuwa kiwakilishi cha wokovu, ushindi, rehema, tumaini pia umekuwa ishara ya Yesu Kristo na pia kanisa maana watu waonapo msalaba umechorwa mahali popote ujua kuwa mahali hapo kuna mkristo au ukristo, wakristo wametumia alama za misaraba katika makanisa, nyuma zao kuonyesha au kukili mbele za watu juu ya Imani yao, wengine wamevaa shingoni na hata wengine kuchora katika mavazi yao. Hakika msaraba umekuwa na uhusiano na muunganiko mkubwa na maisha yetu pia na mwokozi wetu Yesu Kristo. 

 Lakini kabla ya Bwana Yesu kusurubiwa na kufufuka msalaba haukuwa na maana nzuri kwa mwanadamu yeyote kama leo hii, ulitisha na kuogopwa na wote na hakuna mtu  ambaye alitaka kujihusisha nao kabisa.

Askari wa kirumi wakitundika watu misarabani pembezoni
mwa njia.
                                                                                                                                                                                                                                
KIFAA CHA MATESO
Msaraba hapo zamani ulikuwa ni kifaa kilichotumika kutesea watu kabla ya kufa, mtu alitundikwa msarabani akiwa hai na kugongelewa misumari mitatu pekee kwenye viganja viwiri vya mikono na miguu ukusanywa na kugongelewa pamoja, hakika yalikuwa mateso sana kwanza ile misumari uliyogongelewa pia ni pale ukisimamwishwa maana mwili mzima ubebwa na misumari mitatu mikubwa iliyokuwa mikononi na