Waandishi wa Agano jipya kamwe hawakusitasita kuheshimu na kuiinua nafsi ya tatu ya utatu mtakatifu (trinity), na wamekuwa wakirudia kusisitiza umuhimu wa kuishi ukiwa na uhusiano naye. Kasehemu moja, Yesu anawaambia wanafunzi wake kuwa ni kwa ajili yao na faida yao kuwa yeye awaache na kurudi mbinguni ili kwamba aweze kuwatumia Roho Mtakatifu (Taz Yohana 16:7). Hakika hii gharama na kujitoa kwa ajabu kwa umuhimu wa huduma ya Roho! Yesu kwa kusema hivyo alikuwa akimaanisha kwamba ni bora kuwa na Roho Mtakatifu kuliko kuwa na mwana wa Mungu katika mwili (personal)! Yesu alibidi kuondoka ili Roho Mtakatifu aweze kuja, kwa maneno mengine tena ni kuwa ilibidi Yesu kujitenga na wanafunzi wake mwilini ili Roho Mtakatifu aje, kuwa na Yesu mwili siyo bora kuliko kuwa na Roho Mtakatifu.
![]() |
Roho Mtakatifu anahitaji kuwa karibu na wewe katika maisha yako. |