Friday, 1 January 2016

IJUE SIRI YA GIRLFRIEND NA BOYFRIEND -1

     

UTANGULIZI

"Mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa injili ya Kristo" 
(Wafilipi 1:27)

Na ashukuriwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, yeye aliyeniwezesha kuandika somo hili. Somo hili litakuwezesha na kukusaidia kuelewa undani wa Girlfriend na Boyfriend na kuona njia ipasayo ya uzima. Vijana wengi siku hizi huambiana nakupenda lakini hawajui nini maana halisi ya UPENDO au huambiana hivyo kiunafiki tu. Ni vema ufahamu utaratibu wa mapenzi jinsi ulivyopangwa na Mungu katika maisha yako. Maana huo utaratibu umewekwa ndani ya moyo wako tangu enzi, na wengi hawafahamu jambo hili. 

 “Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake tena ameifanya hiyo milele ndani ya mioyo yao , ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya tangu mwanzo hata mwisho."
(Muhubiri 3:11)

KWA NINI MUNGU AMEUMBA TOFAUTI ZA JINSIA?

Tendo la kujamiiana au tendo la ndoa limewekwa na Mungu mwenyewe kwa makusudi maalum na kwa utaratibu mzuri kabisa. Mungu