Thursday, 10 December 2015

MJUWE ADUI WOGA

 

Katika maisha kuna mambo mengi sana ya kutisha na kuogopesha lakini nakuambia ndugu yangu usiogope.

Kimsingi neno "USIOGOPE" katika Biblia limeandikwa zaidi ya mara 360 hii ina maana kila siku Mungu anakuambia usiogope kwa kuwa mwaka  unazo siku 360, hivyo usikubali hofu isikutawale. Woga siyo hali bali ni roho kamili tena ya haitokani na Mungu na kisicho cha Mungu ni cha Shetani ukisoma  2 Timotheo 1:7 inasema:

"Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi"

Hivyo woga ni roho kama ilivyo roho ya umaskini, uasherati & uzinzi, wizi, uchawi, uongo na mengine mengi na mwenye kuipa nafasi roho ya woga kumtawala hakika ataukumiwa tena hukumu yenyewe ni moto wa Jehanamu, hebu soma andiko hili la Ufunuo 21:8 linasema:

"Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili"

Tunaanza kuona mtu wa kwanza kutupwa motoni (Jehanam) ni Mwoga na tunaonyeshwa woga ni dhambi tena sawa na dhambi ya kuchukiza watu, kuua, kuzini, kufanya uchawi, kusema uongo na nyengine. Unaweza uchukie wachawi na kumbe upo sawa nao yaani waendapo na wewe uliye na woga utaenda tu hata kama unafunga na kuomba hata kwenda kanisani, andiko hili linatuonyesha mwenye pepo kwa maana ya roho ya woga au mwenye woga ni sawa na mtu hasiye mwamini Yesu maana hasiye mwamini Yesu atakapo kuishia na mwenye woga ataishia hapo.

Bwana Yesu mara nyingi alipoona wanafunzi wake wana hofu au woga aliwaambia wawe na amani tu, 

"Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga"

Yohana 14:27)



SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI

Kila mtu duniani anayomatatizo na hakuna chanjo ya kutokupata matatizo. Utapata chanjo ya kutokupata kifadulo lakini chanjo ya matatizo huwezi kupata. Hata ukiangalia kwenye ule ulimwengu ulioendelea unaona watu wamejipanga mstari wakiwa na matatizo mpaka unajiuliza “ninyi si ndiyo mmeandaa elimu, kina Isac Newton, Kelvin, Albert Einstain walitoka kwenu? Mbona mnamatatizo?”. Lakini unatakiwa ujuwe kuwa matatizo huwa hayaangalii Teknolojia, Uchumi, Mama mwombaji au mtu alivyo kama uwezo wa mtu, akili za mtu, umaarufu wa mtu au ni nani bali matatizo umpata kila mtu. Matatizo uendelea kuja kwa mtu mpaka pale vyanzo vya matatizo vitakapoondolewa kabisa. Je vyanzo vya matatizo kwa watu ni nini hasa? Watu wengi usema ni Shetani kwa namna ya haraka ila ukichunguza kwa undani si shetani hasa ila ni wanadamu wenyewe ujitengenezea njia ya kuingia kwenye matatizo na uzuni  zitokazo kwa shetani. Tukisoma Biblia tunakutana na maneno 

"Sasa basi, hakuna hukumu ya adhabu juu ya walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.”
(Warumi 8:1)

Tunaona kuwa kuna hukumu ipo juu ya wanadamu ila kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu hawana hukumu juu yao kwa kuwa kuna Roho ya uzima inayokaa ndani yao na kuwaweka huru.

Katika andiko hili tunaona vitu vitatu vya msingi ambavyo ni    
a) Sheria ya uzima
b) Sheria ya dhambi 
c) Sheria ya mauti

Hizi ni sheria tatu za muhimu sana kuzijua na hakika hazipingiki zinaenda kama zilivyo daima. 

Je sheria ni kitu gani?

SHERIA
   Kimsingi kitu kinapoitwa sheria upende au usipende kitakwenda kama kilivyo kwa sababu ni sheria. Hata ulimwengu tunaoishi unaongozwa na sheria au kanuni ndiyo maana kuna sheria nyingi kama vile sheria ya mvutano hapa duniani. Kwa mfano katika sheria ya mvutano tunasema kuwa kitu chochote ambacho kina tundu na hewa katikati kinauwezo wa kuelea mfano puto, dumu, meli au ndege ambayo uelea angani japo imeundwa kwa vyuma ila kwa kupitia sheria ya kuelea uweza kuelea na pia kwa mfano unapochukua jiwe na kuliachilia toka mkononi uanguka mara moja na uweza kujiuliza swali kwa nini jiwe ilo lisibaki likielea angani baada ya kuliachia ila likaanguka chini? Na je ni nini kimefanya jiwe hili kuanguka chini? Ukiangalia kwa makini unagundua kuwa ipo nguvu ambayo uitwa nguvu ya mvutano ambayo uvuta jiwe hili na kutoliacha libaki likielea angani ambapo kwa asili nguvu hii ndiyo uitwa sheria ya uvutano, hii inasukuma vitu viende chini daima na ndiyo maana ukiachia jiwe uenda chini na hata kama jiwe hili ukilirusha juu sana huwa litaenda juu huku likivutwa mpaka litafika mahara na kurudi chini kutokana na nguvu ya sheria ya mvutano ambayo ipo duniani. Na sheria ikiwepo huwa haibishaniwi mfano sheria hii ya mvutano haiwezi kubishaniwi na ukikataa kuibishia sheria hii ya mvutano basi nenda katika jengo refu lolote na ukaluke kutoka juu ya jengo hilo na utakapoanza kuluka hakika utagundua kuwa hauta endelea kuruka kwenda mbele bali utavutwa na kitu usicho kijua kuelekea chini na kuanguka mpaka chini ya jengo hilo na kichwa kilicho pasuka na ubongo uliomwagika ndiyo utasema hakika kuwa sheria ya mvutano ipo. Na ndiyo maana uwezi kubishana na sheria panapofika wakati kitu kinaitwa sheria kinakuwepo ili kiende kama kilivyopangwa, kwa mfano wasomi wa fizikia usema "The small the area, the big the pressure, the big the area, the small pressure" yaani “Udogo wa eneo, ukubwa wa mgangamizo na ukubwa wa eneo, udogo wa mgandamizo” ikiwa na maana eneo linavyozidi kuwa kadogo ndivyo mkandamizo unakuwa mkali zaidi na eneo linapokuwa kubwa ndiyo mgandamizo upungua ndiyo maana n'cha ya sindano ina choma alaka zaidi kwa sababu eneo lake la mbele ni dogo sana hivyo msukumo huwa ni mkali. Pia kuna sheria mbalimbali za asili (nature laws) kwa mfano kuna sheria ya hali ya hewa ambayo inasema kwa kadili unavyoenda juu ndivyo unavyokumbana na baridi na kadri unavyozidi kushuka chini ndivyo unakumbana na joto na ndiyo maana kuna mikoa yenye baridi hapa nchini na kuna mikoa pia yenye joto na hii ni kwa sababu kuna mikoa ipo juu na mikoa mingine ipo chini ya usawa wa bahari hivyo utofautiana hali ya hewa, Sheria hii inatenda kazi ulimwenguni mwote. 

    Sheria kama hizi hakika  huwezi kuzigeuza hata kama ungefanya nini, uwezi kuzigeuza zitabaki kuwa hivyo hivyo siku zote na sharti ni kuzifuata tu, sheria huwa hazibadiliki huwa zinabaki kuwa hivyo hivyo na ukishindana nazo zitakuswaga uingie katika mkondo wake.

   Pia ili nchi iwe vizuri lazima kuwe na sheria na kanuni zenye kuongoza watu wanchi hiyo kwa mfano, kwa nini magari hayagongani barabarani ovyo? Jibu ni kuwa kutokana na sheria za inchini kwetu ambayo uruhusu magari kuendeshwa upande wa kushoto tu ili kuwepo na utarabibu mzuri wa magari kupishana ili yasiweze kugongana, sheria hii usema mwendeshaji aendeshe gari upande wa kushoto wa barabara na hatakama mwenzake akiendesha kulia na kuzidi kumfuata zaidi yeye anapaswa kuendesha kushoto tu, kushoto, kushoto, kushoto tu (keep left), hii ni sheria na ndiyo maana magari yakigongana uonekana jambo la ajabu na watu ushangaa. Hii ndiyo sababu watu wakigongana tu utoka nje ya gari na kitu cha kwanza ni kuangalia gari jinsi lilivyoumia na cha pili ni kuangalia nani kavunja sheria. Na anapokuja askari wa usalama wa barabarani uangalia nani kavunja sheria na ndipo watu usema kupima ajari.

    Kanuni na Sheria zina nguvu na ndiyo maana duniani kuna watu wamewekwa kuwa wasimamizi wa sheria yaani "Law Enforcer" ambapo watu hawa kazi yao ni ukuipa sheria ya nchi nguvu ili watu waifuate na mfano wa watu hao ni kama Polisi, Mahakimu na Askari Magereza. Mapolisi kazi yao kubwa ni kuwanyemelea wale wote wanaovunja sheria, kuwakamata na kuwapeleka katika vyombo vingine vya kusimamia sheria na wakimpata mtu kavunja sheria uchukua maelezo ya jinsi alivyovunja sheria na mashahidi kisha uwapeleka mahakamani na unaweza kuwauliza Polisi “kweni hizi sheria ni zenu?” na watasema sheria hizo ni sheria za nchi na wao wamewekwa kusimamia wanaovunja sheria na kuwakamata na kuwapeleka mahakamani ambapo huko kuna mtu mwingine amewekwa kusimamia sheria ambaye ni hakimu na hakimu huyu ni mtu ambaye amesomea sheria za nchi na kujua mtu akivunja sheria hii adhabu yake ni nini, hakimu yeye amewekwa kusikiliza kesi, kutafsiri sheria na kutoa maamuzi kulingana na sheria ya nchi, mtu akikutwa ni mvunjaji wa sheria kutokana na ushaidii na maelezo yaliyotolewa kwa hakimu basi hakimu utoa hukumu kwa mvunja sheria huyu kulingana na sheria alizovunja na kama ni kulipa faini atalipa au kama ni kutumikia kifungo basi atatumikia na ikiwa hukumu ni kifungo hakimu uangalia sheria ya nchi iliyovunjwa na mda wa kifungo chake na kisha umtolea hukumu hiyo kama ni kifungo cha miezi sita, mwaka au miaka na akisha mtolea hukumu mtu huyo uchukuliwa na askari magereza na kupelekwa sehemu nyengine ya kusimamia sheria ambayo uitwa gereza. Huku gerezani kuna watu wamewekwa na serikali wanaitwa askari magereza hawa kazi yao ni kupokea na kuwatunza kifungoni wale wote waliovunja sheria kwa mujibu wa mahakama na kuwapa kazi wale wote ambao mahakama imesema kuwa ni wavunjaji wa sheria na wanastahili kifungo. Kupitia sehemu hizi tatu tunaweza kuona sheria ya nchi inakuwa na nguvu na kusimama imara na watu uweza kuifuata kwa kuwa vyombo hivi na watu hawa usukuma watu kutii sheria ya nchi.

SHERIA ZA MUNGU

"Neno la Mungu ni Sheria ya Mungu"
Kwenye Biblia pia kuna sheria kama tulivyoona hapo mwanzo katika kitabu cha Warumi 8:1 kuwa kuna sheria ambazo tumeziona za aina tatu ambapo sheria hizo ni Sheria ya uzima, sheria ya dhambi na sheria ya mauti na zote zina wasimamizi wake wenye kuzitia nguvu na hivyo usimama kufuatilia watu wanaovunja waadhibiwe kwa mfano mzuri unapovunja sheria ya nchi hakika polisi wapo, wanakukamata na kukupeleka mahakamani na mahakamani wanakusomea kifungu cha sheria ulichovunja na hakimu anaanza kutafsiri kifungu cha sheria chenyewe na kisha ukipatikana na hatia unahukumiwa kama ni kulipa fedha au kutumikia kifungo na kwenda gerezani na ndivyo ilivyo kwa sheria ya uzima, sheria ya mauti na sheria ya dhambi.

SHERIA YA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI

Sheria ya uzima na Sheria ya dhambi na mauti zina asili zake ambapo kwa sheria ya uzima asili yake ni kuvuta watu kwenda juu daima, lakini sheria ya dhambi ni kuvuta kwenda chini daima, sheria ya dhambi na sheria ya mvutano hufanana, yenyewe ni kuvuta kwenda chini tu. Sheria ya uzima inapovunjwa kama ulikuwa pahali pa juu basi unavutwa na kuelekea sehemu ya chini na sheria ya dhambi lakini bado unakuwa hai ila umeshuka chini kwenye maeneo furani katika maisha yako na ukiendelea kuvunja nyengine unazidi kuvutwa chini tena na tena japo unajiona uko sawa ila kiukweli umeshushwa chini katika maeneo yote kama kwenye kiwango cha mapato, furaha, amani, afya na viwango mbalimbali na ndiyo sababu sasa kuna watu wengi duniani uzuni yao ni kuwa waliwahi kuvunja sheria ya uzima na kufanya sheria ya dhambi ambayo yenyewe inavuta watu toka juu kwenda chini hivyo kujikuta akitelemka chini pasipo kujijua na kukuta maisha yake yamejaa uzuni kwa mfano kama ambavyo sheria ya nchi ina "law enforcer" ambao ni polisi na hao kazi yao kuu ni kuitia nguvu sheria kwa kuangalia wavunja sheria na kuwakamata ili wapate kuadhibiwa sawa sawa na kosa walilofanya kwa kuvunja sheria usika. Mungu naye anazo sheria zake kaziweka, kwa mfano Mungu amesema usiibe, usiseme uongo, usizini, usishuhudie uongo, waheshimu baba na mama yako, usiue na mambo mengine mengi kwenye maandiko yake, sasa unapoiba, unapozini, unapofanya uasherati au unaposema uongo kinachofanyika pale unapofanya hiyo dhambi tu yaani unapoivunja tu sheria ya uzima na kufuata ya dhambi huwa kuna polisi wa kiroho ambao wanaitwa mapepo ambao hawa wanajua sheria ya Mungu na Sheria ya Mungu ni neno lake ambapo ni Biblia kwa mfano Biblia inasema:

"Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu"
(Warumi 6:23)


JINSI MTU ANAVYOPATIWA MSHAHARA WA DHAMBI

Kuna kitu nimejifunza kwenye maisha yangu kuwa kuna kitu mtu unaweza ukawa unafanya kwa siri na hakuna mtu anajua ila ikifika siku ya mshahara watu wote wataona ukipokea mshahara wa kitu hicho ulichofanya silini ila hawatajua ni mshahara wa kazi gani uliyowahi kufanya mpaka ukapata mshahara huo na watakuwa wakishangaa tu na kusema: "jamani kavunjika mguu kabisa?!!" au "jamani mbona alikuwa mtu mzuri kwa nini kapatwa na mambo mabaya?" Shida ni kuwa kazi iliyokupa mshahara huo uliifanyia sirini na wao hawakuijua na kushangaa mshahara umetokea wazii. Kumbe katika ulimwengu wako wa siri kuna jambo ulifanya na sasa umekuwa ukitafutwa kugawiwa mshahara na umekwepa-kwepa mshahara wako hatimaye umenaswa na kugahiwa mshahara wako wazi-wazi mfano kupooza, kufukuzwa kazi, kuharibu mimba, umaskini, kuachika na mambo mbalimbali, ndugu wanaweza kushangaa na kusema: "Shangazi yangu alikuwa mzima kabisa yani jana kaanguka ghafla na kapooza, shetani ushindwe kabisa" kumbe huo ni mshahara wa yale aliyotenda mwaka jana, mwaka juzi au siku yoyote ya nyuma amepatiwa siku hiyo. Andiko linasema:
"Kama vile mtu anapoukumiwa kifo ndivyo
mwenye dhambi pia anavyo hukumiwa"

“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
(Warumi 6:23)

Andiko hili la Warumi 6:23 limegawanyika katika vipande viwili ambapo ni Mshahara na Karama. Neno karama kwa biblia ya kiingereza uitwa "gift" yani zawadi hivyo kwa maana nyengine andiko hili usomeka

 "mshahara wa dhambi ni mauti bali zawadi ya Mungu ni uzima katika Yesu Kristo" 

TOFAUTI YA MSHAHARA NA ZAWADI

 Kuna tofauti kati ya mshahara na zawadi. Mtu anaweza kuahidiwa na mtu kupatiwa zawadi na hasipatiwe  na asidai maana zawadi huwa haiombwi bali mtu utoa kwa jinsi ambavyo moyo wake unampa ila mshahara mtu usipompatia mshahara wake hakika atakudai kwa nguvu zake zote na hata kuandamana hata kwa kubeba mabango maana mshahara ni haki yake kwa kuwa kuna kazi aliifanya na anaitaji malipo yake ya utumishi aliotumika. Mshahara ni lazima mtu aupate, upende au usipende, ulie au usilie lazima ulipwe mshahara kwa sababu mshahara unatokana na kazi uliyofanya au kibarua kuanzia siku ya kwanza ya pili, tatu, nne na mwisho wa mwezi unategemea mshahara umetoka na utapatiwa, vivyo hivyo mshahara wa dhambi ni mauti yaani kifo maana atendaye dhambi ufanya utumishi na utumishi huo ni utumishi wa dhambi na hakika ipo siku lazima aje kupatiwa mshahara na mtoa mshahara sawa na andiko hili:

“Hamjui ya kuwa kwake yeye amaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.”
(Warumi 6:16)

Kimsingi anaposema utii katika andiko hilo ana maana ya utii wa sheria ya Mungu yaani sheria ya uzima ambapo kiongozi wa sheria hiyo ni Mungu na anayeshika sheria zake anakuwa anatumika kwake na lazima siku ya mwisho kutokana na utumishi wake atapata mshahara wake ambapo ni uzima na haki ila kiongozi wa dhambi ni shetani na mtu anapotenda dhambi anakuwa anatumika katika sehemu ya shetani na hakika atakuja kupatiwa mshahara wa utumishi wake wa dhambi ambapo mshahara wa dhambi kwa mujibu wa Warumi 6:23 ni Mauti, na mtoa mshahara huu ni shetani mwenyewe ambaye mtu amemtumikia katika dhambi maana huwezi kufanya kazi wizara ya elimu na kulipwa mshahara na wizara ya maji bali wizara ya elimu ndiyo itakupatia mshahara wako na ndivyo ilivyo ukitumikia dhambi hakika mkuu wa dhambi shetani ndiye atatoa mshahara na mshahara wa shetani ni mauti na si Mungu atatoa mshahara huo kwa mtenda dhambi hakika.

Ndiyo maana wakati mwingine unaweza ukamsikia mtu amekufa ghafla na ukasema: "jamani! yani aiseee!! mbona watu wa Mungu wanakufa ghafla?" hujui kumbe ni mshahara wake wa dhambi alizotendaga kwa siri. Mtu anaweza akavunja sheria ya uzima na akachelewa kutengeneza na Mungu na hivyo waleta mshahara wakamkuta akiwa amevunja sheria ya uzima na kumpatia papo kwa papo.

Maisha ya sirini ya mtu niya muhimu sana maana kesho ya mtu utegemea leo umefanya nini na unachofanya leo cha muhimu sana kitategemea utakuwa nani kesho, pia leo yako ndiyo hakimu wa kesho yako na utakavyo fanya leo ndiyo itaongea utakuwa nani baadaye. Kimsingi hataka kile unachokifanya kama ni kizuri au kibaya na hata kama hakuna mtu anayesema asante au mtu anayesema umekosea hakika kesho kuna kibaya au kizuri kitakupata kulingana na ulivyo tenda leo kwa siri. Unachofanya leo ndiyo mbegu ya mema yako ya kesho au uharibifu wako wa kesho. Kila kitu unachofanya leo kwa mtu hama kwa siri na yeye hajui ikiwa unamsengenya, unamtukana, unamsemea uongo, unamchafua au kumtendea mabaya yeyote kwa sirini hakika unajitendea mwenyewe hakiba ya mabaya siku za usoni. Msiba wa mtu wa kesho unategemea amezalau wangapi mwezi uliopita, amenunia wangapi, amewapiga vita kwa sirini wangapi, ametukana wangapi mwaka huu na mengine mengi yaliyo mabaya.

Ni vizuri kila mtu kushugulika na mambo yako mwenyewe maana kila mtu atasimama mbele za Mungu binafsi na ndiyo maana Yesu akasema msihukumu msije mkahukumiwa maana ukihukumu leo kesho unakuja kuhukumiwa wewe na kipimo kile-kile unachopima ndicho utapimiwa wewe, kipimo upimiacho jirani yako usishangae kesho watu wakaja wakakupimia na wewe hicho-hicho na ukaanza kushangaa na kuomba msaada kumbe uliwahi kupimia mtu au watu siku za nyuma. Watu hawaangushwi na mambo makubwa ila wanaangushwa na mambo madogo madogo ya kila siku.

   Mungu niwa haki unaweza ukafanya kitu leo na ukawa na furaha ya ajabu ila juwa kule unakokwenda kutakuja kubana na utashindwa kupita na wengine watashindwa kujua kwa nini kumebana na kuanza kuomba Mungu kufunguke na utaombewa kanisa kwa kanisa, mchungaji kwa mchungaji kumbe kuna jambo silini umefanya na unaogopa kumwambia mtu na hata ukiomba unaomba chini chini ili mwingine hasisikie maana ni jambo la ajabu ila mwambie Yesu kuwa una siri ndani ya moyo wako na inakukula na kufanya hatua zako zisiende mbele katika sehemu mbalimbali za maisha akusaidie.

SHERIA YA DHAMBI


"Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu"
(Warumi 6:23)

"Tazama roho zote ni mali yangu, na kamaile  roho ya baba ilivyo mali yangu ndivyo roho ya mwana pia ni mali yangu, roho ile  itendayo ndambi itakufa" 
    (Ezekieli 18:4)

KWA NINI KILA ROHO ITENDAYO DHAMBI ITAKUFA?

"Mshahara wa Dhambi ni Mauti"
Hapo mwanzo shetani hakuwa adui wa Mungu bali ni malaika na alikuwa mbinguni akimtumikia Mungu kama mmoja wa malaika zake na alikuwa mzuri kwa mda furani na alikuwa akiifuata na kusimamia sheria za Mungu  ila ikafika wakati shetani akaasi sheria ya Mungu na kufukuzwa mbinguni na uso wake ukageuka akawa siyo malaika tena ila shetani na malaika waliomfuata kuasi naye wakatupwa pamoja naye hapa duniani pahala paitwapo kuzimu na ukisoma katika kitabu cha ufunuo utaona kikisema:

"kulikuwa na vita mbinguni ; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nap pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye’"   (Ufunuo 12:7)

"Shetani alishukua kutoka mbinguni
na malaika zake"
Hivyo shetani alishuka na mabillioni ya malaika hao waasi wenzake ambao ndiyo uitwa mapepo, mashetani, mizimu, majini au roho chafu na kutokana na wingi wao wameweza kuwepo kila mahali duniani na kuijaza duniani chumba kwa chumba, nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, mji kwa mji, nchi kwa nchi na bara kwa bara na hata mahali ambapo uwezi kutegemea kama mashetani hawa hawapo unakuta wapo iwe ni porini, barabarani, jangwani, njia panda au sehemu yeyote. Sheria ya Mungu iko wazi kwa shetani anaijua na mtu anapoivunja tu yeye ugundua ni ipi ilivunjwa kwa mfano mtu mtu aliyeokoka ni tofauti sana na mtu ambaye hajaokoka maana aliyeokoka ameamua wazi kufuata sheria ya Mungu hivyo akitokea kaivunja shetani huwa na nguvu kubwa ya kuleta mabaya kwake kwa mfano mtu huyo akikwazwa na mtu au kitu na akawa na hasira na akaamua kitu ambacho si sawa kwa Mungu kama kumwazia mabaya aliyemkwaza, kumnenea maneno yasiyo mazuri, kumlipizia kisasi au jambo lolote hakika ni kosa maana sheria ya Mungu ambayo ameamua kuifuata inasema haya juu ya kuwa na hasira:

“Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwee na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi”
(Waefeso 4:27)

Maana ya andiko hili ni kuwa mtu anaweza kukasirika kwa kukasirishwa na mtu ila hasira yako isikupeleke kutenda dhambi maana dhambi ni mlango ambao Shetani anatumia kuingilia maisha ya mtu hivyo kutenda dhambi ni kumpa Shetani nafasi na kuto kutenda dhambi ni kumnyima Shetani nafasi kwenye maisha yako. Kimsingi Shetani anakuwa hana nguvu kabisa  kama watu wote wataishi sawa sawa na sheria ya Mungu, shetani anakuwa na nguvu pale sheria ya Mungu inapovunjwa na Shetani sasa ameshushwa hapa duniani katika shimo la rohoni liitwalo kuzimu akiwa na mabilioni ya mapepo hata uwezi kuyahesabu na wamegawana kazi mbalimbali juu ya nyumba, mtaa, mji, nchi au bara usika wakiangalia nani anavunja sheria kamani chumbani, ofisini, barabarani, ofisini, mashambani na sehemu mbalimbali ili wapate kumshitaki na kumpa mshahara wake. Wao wanajua Biblia na sheria zilizopo ndani yake hivyo unapozivunja wao ujua umevunja ipi na ipi na kama wewe ni mkristo nao ujua kuwa wewe ni mkristo na umeokoka na ukitokea kuvunja sheri ya Mungu wao ujua kuwa kitabu chako kinasema usiibe, usizini, usifanye vita na watu kwa siri na mengine mengi, sasa kazi ya mapepo hawa ni kufuatilia vitu hivi kwa kuangalia ni mahali gani sheria ya Mungu imevunjwa ili kukushitaki na kukuletea mshahara wa dhambi ambao ni mauti. 

Kimisingi shetani huwa haendi maala kama hakuna kibali cha kuiba, kuchinja na kuharibu na kama akifika mahala na kukuta hakuna kibali cha kuiba, kuharibu na kuchinja huwa hawezi  kukaa yeye na mapepo wake daima, maana pahala ambapo hakuna kibali cha kuchinja, kuharibu na kuiba ni pahala ambapo Mungu amepahatamia pekee na ndiyo maana katika kitabu cha Yohana tunakutana na andiko lisemalo:

“Mwivi haji ila kuchinja, kuharibu na kuiba”
(Yohana 10:10)

"Tangia atupwe duniani Shetani
amejaa ghadhabu na asila"
Kule kusema “mwivi” maana yake ni Shetani ambaye ndiye mwizi wa afya, masomo, biashara, familia na maendeleo na pia andiko linaposema “Mwivi haji ila kuchinja, kuharibu na kuiba” ina maana pasipo kuwa na kazi ya kuchinja, kuharibu na kuiba huwa Shetani hawezi kuja kabisa kama mwizi wa kawaida hasivyo weza kwenda pahala kama hakuna cha kuiba na uwezekano wa kuiba.

Mungu kwa kawaida huwa anawalinda watu wote lakini inafika wakati Mungu anakosa namna ya kuwalinda. Mtu ambaye amempa Yesu maisha yake na kuokoa hakika mtu huyo ni mwana wa Mungu na kama mwana wa Mungu ni mrithi wa uzima hivyo Mungu uweka ulinzi wake kwa mtu huyo na ulinzi wa Mungu ni kutuma malaika zake kuzunguka watoto wake na watumishi wake siku zote ili mwovu shetani na malaika zake waovu wasiwe na nafasi ya kuwashambulia kabisa, hivyo unapookoka swala la ulinzi Mungu usimamia kwa kuachia malaika zake ambao hao huwa watumishi wetu tunaweza kuona haya katika maandiko aya:

“Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu” 
(Waebrania 1: 14)

                 “Malaika wa BWANA hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa”           (Zaburi 34:7)

 Na pia katika watu walimpokea Yesu Kristo kuwa mwokozi wao na kiongozi wao hakika Mat:

“Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.”
 (Warumi 8:1)

Hivyo tunaona walio katika Kristo Yesu yaani walio na Yesu kwa maana wamempokea na kuokolewa hakuna hukumu kwao juu ya ile sheria ya dhambi ambayo waliivunja zamani kwa kuwa sheria ya Roho wa uzima yaani Roho wa Yesu Kristo mwenye uzima amewaweka huru juu ya sheria ya dhambi na mauti maana dhambi kwa haipo hivyo shetani ambaye ndiye mwivi hana nafasi ya kuja kuharibu, kuiba au kuchinja kwao na watu hawa wanakuwa na ulinzi wa kimungu ambapo Mungu uwatuma malaika zake ambao ufanya vituo kwa watu hao wakiwazunguka usiku na mchana kuwalinda na mwovu shetani na wakala zake mapepo na wachawi na watu hawa uwa salama daima 

"Mtu aliyempokea Yesu hakuna hukumu kwao wapo
pamoja na Mfalme wa Amani Yesu Kristo usiku
na mchana"
Lakini mtu ambaye amempokea Yesu yaani mwana wa Mungu aliyeokoka akitokea akatenda dhambi kwa kuvunja sheria ya Mungu ambayo ni neno la Mungu ndipo Shetani na mashetani wake ambao ndiyo walinzi au wasimamizi wa kuangalia wavunjaji wa sheria za Mungu ili kuwapatia mshahara wa mauti umtazama na kumgundua na kujua ni sheria gani ambayo ameivunja maana wao nao wanaijua sheria ya Mungu kama hapo mwanzo tulivyoona kuwa waliwahi kuishi wakiifuata ila wakaja kuasi hivyo uijua kuliko hata wanadamu na wanapoona umeivunja uanza kukufuatilia na wakija kwa mtu ambaye alikuwa na Yesu na akavunja sheria ya Mungu ukutana na ulinzi wa kimungu na huu huwa unakuwepo kwa kuwa Mungu upenda wanadamu :

“Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu, Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu Wala kuwahuzunisha.”   (Maombolezo 3:31-33)

Hivyo malaika wa Mungu uwa wanaendelea kumlinda mtu huyu hivyo shetani ubeba mashitaka na kupeleka mbele za Mungu ili Mungu aweze kuondoa ulinzi wake ili mtu huyo apatiwe mshahara wa dhambi ambao ni mauti na Biblia ipo wazi juu ya hili kuhusu shetani kuwa anashitakia watu kwa Mungu:

“Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana anetupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.”
(Ufunuo 12:10-12)

Katika andiko hilo juu shetani ndiye anaitwa mshitaki akishitakia watoto wa Mungu usiku na mchana na hii ndiyo kazi yake. Unapovunja sheria ya Mungu shetani upata nguvu na ujasiri wa kutenda kazi yake maana kibali anakuwa amepata maana yeye uweza kwenda pahala penye kuchinja, kuiba na kuharibu hivyo uja na kumwambia Mungu:

“Mungu yule mtu wako aliyeokoka juzi mbona leo kavunja sheria yako ya uzima sasa si nimpatie mshahara wake kwa kuitumikia dhambi ambapo mshahara huo kwa mujibu wa neno lako katika Warumi 6:23? Au na wewe siyo wa haki kama mimi? Je unageuka-geuka kama mimi?”


Sasa Mungu ni mwenye haki na sifa ya mwenye haki ni tatu ambapo ni:

1. Haangalii sura ya mtu wala umbo la mtu wala urefu wa mtu anaangalia moyo
2. Akisema kitu habadiliki
3. Niwa milele

Huyu ni Mungu, na kwa kuwa Mungu ni mwenye haki kwa maana hana kubadilika, hana upendeleo na ameshasema katika neno lake kuwa mshahara wa dhambi ni mauti hivyo hakika mauti hiyo umpata kila mtenda dhambi na msimamizi wa kutoa mauti hii ni shetani ila Mungu ni pendo na anampenda mtu huyo aliyetenda dhambi na anapenda aweze kutubu na kuwa na uhusiano naye tena maana andiko lasema:

“Je! Mimi ninafurahi kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?”
                                                                   (Ezekieli 18:23)

Katika andiko hili tunaona kuwa Mungu hana furaha na kifo cha mtu mwenye dhambi na anasema ni bora angeamua kutubu na kuacha dhambi ili aweze kuishi, haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa mtu mwenye dhambi. Ila mapenzi ya Shetani ni kuua, kuchinja na kuharibu kila mtu  yeye si upendo na wala hana upendo na wanadamu kabisa hivyo usimama kwa furaha kuakikisha mauti inampata mtu huyo na kumwambia Mungu aondowe ulinzi kwa mwenye dhambi ili apate nafasi yeye na mashetani wenzake kumwangamiza na Mungu huwa hajibu kitu bali anakaa kimya kwa uzuni kubwa na shetani kumwambia Mungu yeye ni kweli na kama ni kweli atoe hukumu ya kweli sawa na neno lake na asiwe kama yeye baba wa uongo pia Mungu ni mtakatifu na hana dhambi kama alivyo shetani hivyo hana uhusiano na dhambi wala wenye dhambi na kwa kuwa Mungu ni mwenye haki na malaika wanampenda Mungu na wasingependa kuona shetani akimsema ujisikia kuhukumiwa ndani yao hivyo wanaondoka kwa mtu huyo na ulinzi wa kimungu unakuwa haupo juu ya mtu huyo. 

Siyo Mungu aliyemtuma Shetani kumwangamiza mwanadamu ila Shetani katumia neno la Mungu kuleta mashitaka na kupitia mashitaka hayo amepata kibali cha kuangamiza. Hivyo shetani na malaika zake waovu uanza kumletea mtu mshahara wa dhambi hiyo ambapo ni mauti na kwenye taratibu zake shetani za kuua huwa aleti mauti moja kwa moja ila anaanza taratibu kama kisukari gafla na mtu anapooza na anaendelea kuwa akijivuta na mala kapooza kabisa na kapelekwa hospitali na kulazwa. Sasa ni juu yake huyu mtu kugundua kuwa ni wapi alipoacha upendo wake wa kwanza na atakapo kumbuka na kusema "Baba Mungu nimekosea, nisamehe, nihurumie..." na akarudi kwa Mungu tena ila akinyamaza kimya malipo ya dhambi ambayo ni mauti uendelea kwa sababu mashitaka mashitaka hayabatilishwa kwenye ulimwengu wa roho, yapo na hao mapepo ni mapolisi wa Shetani wa kukamata wahalifu wanaovunja sheria ya Mungu na mwisho mtu huyu anakufa na kuishia dhambini na Shetani kuwa amemaliza kazi. Mungu mbinguni anasikitika sana maana hapendi hata mtu mmoja hapotee.

MBINU ZA SHETANI KUFANYA WATU WAVUNJE SHERIA ZA MUNGU


Adamu na Hawa walipotezwa na Shetani
Shetani uwinda sana wale watu ambao wamekwisha kumwamini Yesu na kumpa maisha yao na wapo katika ulinzi wa Mungu na yeye kutokuwa na uwezo wa kuleta mabaya kwao, kwa watu hawa uweza kutumia njia mbalimbali kama hasira, chuki, wivu, kusengenya, uongo, matusi na mambo mbalimbali, uweza kutumia watu ambao hawana Yesu kuwakwaza watu wa Mungu ili waanze kushindana mwilini na kuufuata mwili kwa mfano umeokoka na umepanda basi na ukiwa katika basi mtu akakukanyaga na ukaanza kumwambia kwa nini amekukanyaga au kumwambia atoe mguu wake juu ya mguu wako na unaye muuliza anakujibu jibu baya la  kukukwaza na unakwazika na kupigana, kutukana au kuamua uamuzi mbaya juu ya mtu huyo basi hapo hapo katika ulimwengu wa rohoni shetani na mapepo ukimbia kwa Mungu na kuleta mashitaka kwa kuwa imeandikwa:

"Kushindana kwetu si juu ya damu na nyama"
(Waefeso 6:12)

Maana ya andiko hili ni kuwa sisi ambao tumempokea Yesu kushindana kwetu juu ya kitu chochote si kutumia mambo ya kimwili au kutumia mwili bari ni rohoni maana mwili na roho zote zina nia ila nia ya mwili ni mbaya siku zote tofauti na nia ya roho ambayo ni njema, maana imeandikwa:

“Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili;bali wale waifuaatao roho . Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.”
                                                                  (Warumi 8:5-8)

Hivyo nia ya mwili siku zote ni mauti ikiwa nia ya mwili ni mauti hii ina maana mwili ulenga dhambi ambapo mshahara wa dhambi ndiyo mauti hivyo mtu afanye vita na mtu au watu kwa kutumia mwili hakika hawezi kutii sheria ya Mungu atajikuta anatenda dhambi tu maana mwili una uadui na Mungu na hauwezi kutenda sheria yake, hivyo shetani upenda kuleta watu kutukwaza au kututendea mambo ili tuwe na hasira na kuamua kushindana kimwili ili tutende dhambi na aweze kutupatia mshahara wa dhambi, pia neno la Mungu linaendelea kusema juu ya kufanya vita kimwili:


"Maana ingawa tunaenenda katika mwilini, hatufanyi  vita kwa jinsi ya mwilili....."
(2 Wakorintho 10:3)


Neno la Mungu ni sheria ya Mungu hivyo utumia neno la Mungu kupata kibali na kuanza kumletea mtu huyu ugonjwa, ajari, kesi na kufungwa au mambo mbalimbali maana ulinzi wa Mungu unakuwa haupo kwake na mtu huyu akiona mabaya haya na kujua kuna pahala kakosea na kumwomba Mungu msamaha na Mungu hapo hapo umsamehe na malaika urudi na kumzingira na mashetani ukimbia na kukosa kibali na mtu huyu kuwa katika ulinzi wa kimungu na kutoka katika matatizo yaliyoletwa na shetani.

Ndiyo maana ni vizuri unapokuwa mkiristo, unapokosea jambo usiruhusu muda kuomba msamaha, ukikosea jambo hapo hapo omba msamaha na hata kama upo kwenye gari paki pembeni na uombe msamaha kwa Mungu maana hujui nini ambacho shetani ameandaa mbele yako, maana kuna uwezekano kwa aliyevunja sheria ya Mungu kutubu na Mungu kumsamehe na mshahara wa dhambi yaani mauti usimpate, andiko hili lipo wazi juu ya hili:

“Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizotenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatajufa. Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi”
  (Ezekieli 18:21-22)

Watu wengine wanamkosea Mungu kwa kuvunja sheria yake na wanaendelea kumwomba Mungu ulinzi kwa kusema kwa jina la Yesu au kwa damu ya Yesu ila kimsingi haifanyi kazi na matatizo ya mtu yataendelea kumpata mtu maana hakuna ulinzi wa Mungu pahala penye dhambi au ushindi wa kimungu kwa shetani kwa mtu mwenye dhambi.

Ni vizuri kabla ya kuomba maombi ya baraka, ulinzi, vita na mambo mbalimbali ni lazima mtu ufanye maombi ya toba au msamaha kwanza hata kama unaona hakuna pahala ulipokosea maana kuna wakati mtu unaweza kuvunja sheria ya Mungu bila kujua na kutokujua kwako hakukupi haki maana hata mahakamani unapovunja sheria na kushitakiwa uwezi kujitetea kwa kusema eti sikujua sheria hiyo ya nchi na ukisema hivyo utahukumiwa tu na ndivyo sheria ya Mungu unaweza kuivunja bila kujua na ukahesabiwa sawa na mwenye kuvunja huku akiiijua, hivyo omba toba hatakama ujui ni wapi ulitenda dhambi ili shetani asiwe na kibali cha kuleta mauti maana anapokuwa na kibali hata kama uombe vipi kwa kuwa anakibali hakuna cha kumzuia maana yupo sawa na kile neno la Mungu linasema yaani mshahara wa dhambi ni mauti.

Pia kila jioni kabla ya kulala ni vizuri mtu kutafakari ni wapi siku nzima ulikosea, kujaribu kuvuta picha ni nani ulimkosea, maneno gani mabaya ulinena, ulimsengenya nani, ulisema uongo wapi na ukigundua ni kumwomba Mungu hapo hapo kwa kumwambia akusamehe kwa hayo uliyotenda naye ni mwaminifu atakusamehe.

Kuna watu udhalau dhambi kwa kusema dhambi hii ni kubwa na dhambi hii ndogo hivyo kutazama zile kubwa na kuzitubu na kuacha dhambi ndogo, kimsingi hakuna dhambi kubwa wala dhambi ndogo zote ni dhambi na dhambi zote zinampeleka mtu motoni japo macho yetu usema hii kubwa na hii ni ndogo ila mbele za Mungu dhambi zote ni sawa na zote hatima yake ni moja.

Ndiyo maana sasa Shetani na wakala wake mapepo hawa ni maafisa wakumkamata mtu aliyevunja sheria na kumpeleka kumpa haki yake yaani mshahara wake wa mambo aliyotenda na ndiyo maana ni vizuri kama mkristo kugundua aina ya maisha unayoishi kwa siku, wiki na mwaka ndiyo mwamuzi wa utakuwa nani miaka kumi, anayeamua utakuwa nani miaka kumi siyo Mungu ila ni wewe mwenyewe na ndiyo maana neno la Mungu linasema "amelaaniwa afanyaye vita na kipofu na alaaniwe" kipofu katika andiko hili ni mtu ambaye hajui au atambui, yeye unampiga vita  hajui, mmekaa mahali mnamwongelea yeye hajui, utasikia "unajua furani anajidai sana..." mara "unajua yule anavaa vibaya..." na anayesemwa hajui, huyo ni kipofu, unaweza ukamsema mtu na asijuwe ila mashetani wanaona na baadae ukajikuta unapatwa na mabaya na hii ni moja ya sababu ya wanawake wengi shetani anakuwa anawaonea sana katika mapepo kwa sababu milango mingi wanakuwa wameweka wazi, milango mingi inakuwa wazi, milango ya maneno, milango ya kuongea, milango ya kuteta, kuna wengine ukimteta hatakama akijua ananyamaza kimya na bahati mbaya mtu unayemteta akiamua kunyamaza kimya ni mbaya zaidi maana anayenyamaza kimya anamruhusu Mungu akutandike ila anayeongea huwezi kutandikwa maana ameamua kusimama mwenyewe. Ukimtukana mtu au kumsema na yeye anaendelea na mambo yake hana mda wa kujibu maana yake amenyamaza kimya na kumwachia Mungu asimame mwenyewe na kuhukumu na Mungu anajua kutoa hukumu ya kweli kuliko mwanadamu. Neno la Mungu linasema "Nanyi mtanyamaza kimya, nami nitawapigania" Ukisikia watu wanaongea kuhusu wewe, kimsingi nyamaza kimya maana utawaona baada ya mwaka mmoja kifafa, kupooza yataanza kumpata usiseme nao hapo wala kushangilia wewe nyamaza mpaka mwisho wao, mfano mzuri Bwana wetu Yesu aliposemwa, alipotukanwa, aliposngenywa na siku aliyokamatwa alipigwa na kuonewa sana ila alipoambiwa na Pontio Pilato akamwambia jitetee na hakujitetea, je ungekuwa wewe si ungejitetea kweli kweli na Pilato alipotaka kumsaidia hatoke na wayahudi kujua na kumpinga kuwa aweze kumsulubisha ndipo Pilato akamuuliza wewe ni mfalme wa wayahudi ila Yesu akanyamaza kimya sasa ingekuwa ni wewe ungejieleza kwa hakimu mwenyewe ila Yesu alinyamaza kimya, akimu Pilato akamwambia haunijui mimi kuwa nina mamlaka ya kukusulubisha au kukuachia? Ila Yesu akasema Hapana, na kusema mamlaka aliyonayo na cheo alichonacho kapewa na Mungu wa mbinguni na Pilato akashangaa sana akasema siwezi kumuhukumu mtu wa aina hii akasema leteni maji ninawe na haijawahi kutokea mahakamani mpaka leo jaji akaomba maji anawe ndiyo haukumu mtu,Pilato akaanza kunawa maji huku akiongea kuwa hana hatia ya damu ya Yesu ila Yesu bado alikuwa kimya tu na baadae akalala msalabani na akakinga mikono, wakapigia misumari kimya ajanena neno juu yao, baadae wakainua msalaba juu bado yupo kimya, hakurudisha neno hata moja bali alipofika juu msalabani akasema "naona kiu. Baba naomba uwasamehe hawajui watendalo" akunena baya juu yao na ilipofika saa sita mpaka saa tisa Yesu akasema "imetosha" ndipo Baba wa mbinguni akaamua kuingilia kati baada ya Yesu kunyamaza kimya mda wote huo japo ametukanwa, amepigwa, katemewa mate, amevikwa taji ya miba ila akawa amenyamaza kimya, amechubuliwa na amechomwa mikononi na miguuni yupo kimya tu ile saa sita mpaka saa tisa Biblia inasema dunia ikawa giza na mawe yakaanza kupasuka na pazia la hekalu likapasuka vipande viwili kwanzia juu mpaka chini na dunia ikatikisika na miamba ikapasuka na makaburi yakafunguka na Yesu akalia kwa sauti kuu akasema "IMEKWISHA" Biblia inasema wale waliokuwa wanamsurubisha walipoona namna alivyokufa wakasema "hakika mtu huyu alikuwa mwana wa Mungu" lakini mameshachelewa Yesu akafa, wanagundua ni mwana wa Mungu amekwisha kata roho na ndiyo maana baadae mitume walipoanza kuhubiri injiri ilikuwa inawachoma kweli kweli na wanaanza kusema 'yule alinyamaza kimya, alikuwa kama kondoo apelekwaye machinjoni, naye hakubisha neno alinyamaza kimya na sisi tu mashahidi wake, na ninyi mlimuua lakini Mungu akamfufua kutoka kwa wafu" wako kimya, nyamaza kimya Mungu mwenyewe akupiganie, nyamaza kimya na Mungu atasimama mwenyewe kukupigania. Kimsingi kubweka siyo kuuma.

Ni vizuri kama mtoto wa Mungu kujifunza kuwa kimya pale watu wanaposimama kukusema vibaya au kukushambulia kwa maneno ya uongo au matusi maana wanadamu ni lazima waongee maana tunaona tokea mwanzo mapaka ufuono wanadamu wamekuwa wakisema vibaya manabii, mitume, waamini na hata Bwana Yesu mwenyewe alisemwa ila wote walikaa kimya. Wanadamu wanasema, uwezi kuwatosheleza wote hata siku moja maana ukijitaidi kuendelea kutenda mema wataendelea kusema tu maana zuri kwa huyu kwa huyu ni baya, unaweza ukawa unaenda kanisani kila siku ukasangaa wana kusema 'anajifanya anaenda kanisani basi kanisa litamchosha tu" na wewe unakwenda tu na baadae ukiacha watasema "Umeona, kanisa awe yeye? Si tulimwambia atachoka tu" na ukisema ubaki nyumbani uwe mwizi watasema tu napo.

Niliwahi kusoma kitabu cha mtu mmoja ambaye anasema "dont please man, you cant please man" mwandishi wa kitabu hiki ndani ya kitabu chake anasema siku moja akulikuwa baba mmoja mtu mzima na mwanaye, mwanaye ni mdogo kidogo ana miaka kama kumi na mitatu na walikuwa na punda wakisafiri, wakiwa wanaanza safari baba akatoa wazo na kumwambia mwanaye "mwanagu kwa kuwa wewe ni mdogo basi wewe panda punda huyu" mwanaye akapanda punda na wakiwa wanaendelea na safari wakakutana na kundi la vijana na kundi la vijana wale wakawa wanasema na waka wasikia wakisema “kijana huyu ni mjinga sana, yaani mzee anatembe kijana limepanda punda? Yani halina akili kabisa, matoto ya siku hizi bwana" yule kijana akasiki na akashuka haraka kwenye punda na kumwambia "Baba panda wewe, umesikia walivyosema" ila baba akauzunika, kijana akashuka baba akapanda na wakaendelea na safari na kukutana na kundi la wazee nao wakasema "mazee ya siku hizi hayana huruma kabisa, yaani mtoto ambaye wala ajala chumvi nyingi anatembea ila zee ambalo hata atuwezi kusema litakuwa rais baadae kwa kuwa limeshazeeka eti kapanda punda na mtoto anatembea" mzee akasikia moyo unamuuma kabisa maana alisikia maneno ya wazee hao na kisha akamwambia mwanaye "panda mwanangu" ila mwanaye akasema "hapana baba, tupande wote" wakapanda wote na kuendelea na safari mbele wakakutana na watu wa haki za wanyama nao wakasema "jamani yani huyu baba na mwanaye hawajui haki za wanyama yaani kipunda kimoja kidogo wamepanda watu wawili? Hawana huruma kabisa" waliposikia baba na mwanaye wakashuka haraka na kusema wamwache punda aende mwenyewe na wakaendelea na safari na kukutana na watu wengine nao wakasema "jamani hawa ni wajinga kabisa yaani wanatembea na punda wanaye? Badala ya mmoja kupanda punda na mwingine akichoka ashuku aliyepanda na asiyepanda apande" yule baba aliposikia akamwambia mwanaye "huwezi kupendeza watu wote" hivyo wakaendelea kama wapendavyo wao na sio watu. Hatuwezi kuwasikiliza watu, hatuwezi kuwasikiliza majirani, hatuwezi kusikiliza watu wote, semeni asubuhi, semeni mchana, semeni jioni na hata usiku mimi nimeamua kumwamini Yesu Kristo, nimeamua kudhalau aibu nina songambele kwa nguvu zangu zote. Hivyo watu wanaweza kukusema vibaya na mambo mbalimbali cha msingi kuwa makini shetani uweza kutumia sehemu hizi tukienda kinyume na sheria ya Mungu.

Ikiwa umetenda jambo kinyume na mtu iwe kwa siri na wewe unajua ni vizuri kumwomba Mungu msamaha haraka.

Kuna ulimwengu wa Mwili na Ulimwengu wa rohoni, ulimwengu wa mwili ni bayana na ulimwengu wa rohoni pia na kama mwilini kulivyokuwa na viumbe mwilini na ndivyo mwilini kunaviumbe pia ambapo kuna mashetani na mapepo na wapo kila pahala ambapo kwa macho ya nyama yani ya mwilini uwezi kuwaona ila kwa macho ya rohoni unaweza kuwaona, wapo kazi yao kuwanyemelea watu wanapokosea sheria ya Mungu ili kuwaletea mshahara wa dhambi ambao ni mauti na ndiyo maana Mwanzo wa shida ya mtu ni dhambi ndiyo maana hata Mwanzoni Mungu alipomuumba Adamu na Eva walikuwa hawafi, hawalimi, hawana magonjwa ila walipotenda dhambi cha kwanza uchi, shida ya mavazi ikaanza

Kama wewe ulikosea alafu bila kujua polisi wa shetani wakakukamata na kukushitaki na kujikuta upo kwenye mashitaka ya magonjwa nataka nikusaidie jinsi ya kuomba ili uweze kumwomba Mungu msamaha kwa jambo lolote ambapo nafsi yako inajisikia kushitakiwa, kuna matatizo unayo ambayo yanatokana na sehemu furani ulivunja sheria ya Mungu na umejitaidi kumwomba Mungu mara kwa mara na kuombewa pasipo kupata utatuzi ni vizuri kusimama mbele za Mungu kwa moyo wa toba na kupasa sauti yako mbele za Mungu kumwomba msamaha kwa ajiri ya makosa  yao yote na Mungu ni mwaminifu hizi ni baadhi ya ahadi za Mungu juu msamaha kwa mwenye kuomba kumwita Mungu kwa toba.

NAMNA YA KUOKOLEWA NA MASHITAKA
 Kumwomba Mungu Msamaha
 "Yesu yupo tayari kukuokoa na kukusamehe
dhambi yoyote uliyonayo maana yeye ni
mkubwa kuliko dhambi zako"
Mungu ni mwenye huruma, Mungu ni mwingi wa rehema. Petro alimkana Yesu mara tatu na alpokuja kutubu Bwana Yesu alimsamehe na kumfanya kuwa kiongozi wa mitume, pia Petro aliwahi kumuuliza Yesu kuwa mtu akimkosa amsamehe mara mangapi na Bwana Yesu akasema saba mara sabini akiwa na maana kumsamehe mara 490 kwa siku, je kama Yesu alimwambia Petro aliye mwanadamu kama mimi na wewe kusamehe mara 490 kwa siku, je yeye Mungu ambaye ni pendo anatusamehe mara ngapi? Jibu ni mara nyingi sana

"Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitendas dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote."
  (1 YOHANA 2:1-2)

Ikiwa kwa maneno yako watu waliumia moyo au kwa ujumbe wako wa simu uliwatumia watu na mioyo ikaanza kuwauma, ukazini, ukasema uongo au kufanya jambo lolote ambalo si zuri machoni pa Mungu na umefanya silini na hakuna aliyekuona au kugundua basi juwa Mungu analijua na Shetani analijua ila Mungu analijua ili akusamehe lakini shetani analijua ili akuhukumu kwa kukuletea mabaya ni bola leo umkimbilie Mungu akusamehe na kukupa haki ya uzima iliyopo kwa Roho wake wa uzima aliye ndani ya mwanaye Yesu Kristo.

Baba Mungu wa Mbinguni, nimegundua yale niliyoyafanya, yamenifanya kuwa mateka wa dhambi na sheria ya dhambi imenivuta kwenda chini, leo ninakataa Bwana, ninaomba msamaha kwa yale niliyotenda, niliyotenda kwa siri bila mtu kujua, ninaomba Bwana unihurumiye kwa maana malaika waovu waliniona na wewe Bwana uliniona na nimeshitakiwa anipo kwenye mashita, na nimehukumiwa magonjwa, nimehukumiwa kushindwa, sasa leo, ninaomba unisamehe ninaikataa hukumu iliyopitishwa juu yangu, kwa damu ya Yesu, hukumu ya kifo, hukumu ya kushindwa ninaikataa kwanzi leo kwa damu ya Yesu iliyomwagika msalabani, kwa damu ya Yesu ninaomba Bwana unisamehe kwa yale niliyoyatenda bila kujua yakanifanya kuwa mateka na leo polisi wote wa rohoni walionikamata leo ninawaondoa kwenye maisha yangu kwa damu ya Yesu, kwa damu ya Yesu, kwa damu ya Yesu.

kwa dakika chache mwombe Mungu msamaha kwa mambo yote ambayo moyo wako unaoona kwamba ni muhimu kumwomba msamaha.......

Umeshamwomba Mungu msamaha na Mungu amekwisha kusamehe ikiwa umeomba maombi haya kwa kumaanisha na kuziungama dhambi zako na mambo yote ambayo moyo wako ulikuwa umeyahifadhi dhani yake na sasa ni mwana wa Mungu na ulinzi wa Mungu upo juu yako na malaika wa Mungu wapo upande wako sasa omba maombi haya ili kuondoa kila ambacho adui alikiweka maishani mwako.

Katika jina la Yesu kristo ninayaondoa mashitaka ya kila aina ambayo shetani na wakala wako mlinishitaki kwa hayo maana Mungu amekwisha nisamehe sasa nawaagiza enyi washitaki katika jina la Yesu, Yesu alisema kama hakuna mtu anayekushitaki na mimi sikushitaki, Yesu alimwambia mwanamke aliyekamatwa na Yesu alimuuliza mwanamke huyo washitaki wako wapi akasema hawapo na Yesu akasema kwa kuwa washitaki wako hawapo na mimi sikushitaki sasa kama Mungu hanishitaki hakuna anayetakiwa kunishitaki, washita ki wa laana, baala, mikosi, magonjwa, mauti, udhaifu nawaondoa katika maisha yangu, wale wanaoniweka ndani ya balaa, mikosi, kukataliwa na watu ninawaamuru kwanzia sasa enyi mashetani wa balaa, mikosi, kukataliwa na watu, magonjwa, umaskini mliokuja kwangu kunisimamia nibaki kwenye umaskini nawaagiza sasa mashitaka hayapo juu yangu tena kwa jina la Yesu ondokeni kwangu kwa jina la Yesu na muachie njia ya maisha yangu kwa jina la Yesu. Achia njia ya baraka, achia njia ya baraka kwa jina la Yesu ni kweli nilikosea ila nilimwomba Mungu msamaha na amenisamehe hivyo nawaagiza mashetani wote mtoweke kwenye maisha yangu na vifungo vyenu viniachilie kwa jina la Yesu Kristo mwana wa MUngu aliye hai toka kwanzia sasa kwa mamlaka ya jina la Yesu, roho za balaa, mikosi laana na kuamuru niachi nimeshasamehewa naamuru kwanzia sasa sipo chini yenu na ulinzi wenu, laana ziame juu yangu mimi siyo mtoto wa laana na mikosi tena ni mtoto wa baraka, laana hama juu yangu kwa jina la Yesu, magonjwa yaliyotokana na dhambi naagiza yahame kwa jina la Yesu. Washitaki wa ndugu nawaagiza hameni kwanzia sasa kwa jina la Yesu. Achia maisha yangu, maisha mlioniwekea ya dhiki yaondoke kwa jina la Yesu. Kupata hasala katika biashara toka kwa jina la Yesu, maisha yangu ya nyooke, familia inyooke, mafanikio yafunguke, fedha ifunguke, magonjwa ya maisha yangu yahame mara moja kwa jina la Yesu.

kwanzia leo wewe ni mwana wa Mungu tembea kwa ujasiri hakikisha maisha yako yanaenda sawa na neno la Mungu ili Shetani asije kupata nafasi ya kukushinda maana neno la Mungu linatuambia:

"Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake"
(2 Wakoritho 2:11)

hivyio kama mwana wa Mungu tambua ya kuwa unaye adui mkubwa aitwaye shetani hapa duniani anakuwinda na kukutamani kukuangamiza ni kama simba angurumaye:

"Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani"
(1 Petro 5:8-9)

Biblia inatuambia tuwe na kiasi, kuwa na kiasi ni kuwa na mipaka yaani angalizo mfano utani ni kitu kizuri lakini usije kupitiliza ukasema uongo maana kuna watu usema uongo kwa kisingizio cha utani na kumbe ni uongo na uongo ni moja ya dhambi ambazo Mungu amekataza na moja ya amri kumi kuwa "usiseme uongo" neno la Mungu linatuambia utani wa namna ya uongo ni mbaya:

"Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge, Na mishale, na mauti; Ndivyo alivyo amdanganaye mwenzake, Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu?"
(Mithali 26:18-19)

Na biblia inatuambia kuna hukumu kwa wenye kupenda mzaha kama hii ya kuwaambia watu uongo, kuchukiza watu (kukwaza), kutukana watu, kusengenya watu n.k

"Hukumu zimewekwa tayari kwa wenye mzaha; Na mapigo kwa mgongo wa wapumbavu"
(Mithali 19:29)
Hivyo Shetani atajitaidi kukusukuma katika mambo yaendanayo na hayo ambayo kwa haraka unaweza usijuwe kuwa ni kosa kwa kuwa hukujua kwa maana hukusoma neno la Mungu na kujua au fahamu zako zinaona si kosa na ukitenda tu yeye kama msimamizi wa wale wote wanaovunja sheria ya Mungu uweza kuanza kutawala na kuongoza maisha yako katika njia mbaya, kuwa na kiasi mtu wa Mungu epuka kufuata makundi ya watu waocvu, usiambatane nao, jiepushe nao usije kujumuika nao ukajumuishwa katika mabaya yao na kuangamizwa nao.

"Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali. Wakisema, Haya!  Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu; Tuwameze hai kama kuzimu, Nawazima, kama wao washukao shimoni. Tuitapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka. Wewe utashirikiana nasi; Tutakuwa na vitu vyote shirika. Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao. Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu. Kwa kuwa mtego hutegwa bure, mbele ya macho ya ndege ye yote. Na hao hujotea damu yao wenyewe, Hujinyemerea nafsi zao wenyewe."
(Mithali 1:10-19)


"Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali Sheria ya BWANA ndiyo imependezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. Sivyo kama walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya mwenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea?"
(Zaburi 1:1-6)

Munga anasema anayo heri mtu ambaye hana ushirika na haambatani na waovu bali siku zote yeye utafakari sheria ya Mungu usiku na mchana, sheria ya Mungu ni neno la Mungu hivyo ni heri kusoma na kutafakari neno la Mungu na kuangaika jkulijua ili kulitenda kuliko kupoteza muda na waovu naposema kupoteza muda na waovu sina maana watu pia vitu vya uovu, watu wengi leo upoteza muda katika vitu mbalkimbali mfano kutazama filamu, tamthilia, miziki, michezo na mambo mbalimbali ambayo kimsingi hayampi Mungu utukufu hata siku moja, ndugu kwa siku unayoi masaa 24 tu na unazo siku saba ndani ya wiki na siku 30 mpaka 31 ndani ya mwezi na siku 360 kwa mwaka si mda mrefu sana hebu tumia muda wako na Mungu katika maombi, kusoma neno na kusikiliza, shuhudia watu na ombea watu usipoteze muda maana tunao muda mchache sana hapa duniani na ubaya hata uchache wake hatuujui maana mda wowote unaweza kufa kwanzia sasa maana hata unaposoma maneno haya kuna maelfu ya watu wanapoteza maisha ulimwenguni. Chukua uamuzi mzuri, soma neno la Mungu na kuluifanyia kazi, Biblia inasema utakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya mto wa maji na utachanua na kuzaa matunda yake kwa wakati na kamwe hauta nyauka, mti huo ni wewe unaposoma neno la Mungu na kulitafakali huku ukilitenda unakuwa karibu Mungu ambaye ni chanzo cha uhai na kila kitu yeye ni kama mto wenye maji safi ambapo mizizi yako itanyonya kwake baraka, ulinzi, ushindi, amani, furaha na vitui mbalimbali na chochote ambacho utapanga kufanya au kuanza kama ni masomo, biashara, familia, kazi vitasitawi na havita nyauka maana Mungu wa baraka atakuwa na wewe. Nakutakia siku njema mwana wa MUNGU. Asante kwa kusoma maneno haya, naomba uyatendee kazi, kwa maswali, ushauri na maombi nitafute kwa anuani hizo chini:

Mwl Judicate Fredy Mnyone
+255765544589
judicatemnyone@gmail.com










Saturday, 20 June 2015



Swali: "Ukristo ni nini? Wakristo huamini nini?"

Jibu: Wakorintho wa kwanza 15: 1-4 inasema, “Tena ndugu zangu, ninawatangazia tena ile injili ambayo nimekwisha kuwahubiri ambayo mmeipokea nakusimama ndani yake; ambayo kupitia hiyo mmeokolewa mkiendelea kukumbuka yale niliyowahubiri msije mkawa mmeamini bure. Kwa kuwa niliwapatia kwanza kile nilichokuwa nami nimepokea, kwa jinsi ile Yesu aliyokufa kwa ajili ya dhambi zetu kulingana na maandiko; na akazikwa, hatimaye akafufuka tena siku ya tatu kulingana na maandiko.

Kwa kifupi hii ndiyo imani ya kikristo. Ukristo ni imani maalum kulinganisha na nyinginezo, Kwa sababu inasimamia zaidi ushirika na Mungu kuliko matendo ya kidini. Kinyume na kushikilia orodha ya masharti ya fanya haya na usifanye yale, Lengo la mkristo ni kutafuta ushirika wa karibu na Mungu Baba. Ushirika huo unawezeshwa na kazi aliyoifanya Yesu pamoja na huduma ndani ya maisha ya mkristo ya Roho Mtakatifu.

Wakristo huamini ya kuwa biblia ni Neno la Mungu na mafundisho yake ndiyo mamlaka ya mwisho (Timotheo wa pili 3:16, Petro wa pili 1: 20-21). Wakristo huamini juu ya Mungu mmoja akaaye katika utatu, Baba na Mwana (Yesu kristo), na Roho Mtakatifu.
Wakristo huamini yakwamba mwanadamu aliumbwa ili awe na ushirika na Mungu lakini dhambi hutenganisha watu wote na Mungu (Warumi 5:12, Warumi 3:23). Imani ya kikristo hufundisha ya kwamba Yesu kristo alitembea juu ya ardhi akiwa Mungu kamili na huku akiwa pia mwanadamu (Wafilipi 2:6-11), na akafa msalabani. Wakristo huamini ya kwamba, baada ya kifo chake msalabani, Yesu alizikwa, akafufuka na sasa anakaa upande wa kuume wa Mungu Baba akiwaombea waumini milele (Waebrania 7:25). Imani ya kikristo inasema ya kwamba kifo chake Yesu kristo msalabani kilitosha kufidia dhambi za watu wote na hili ndilo linalorejeza ushirika baina ya Mungu na mwanadamu (Waebrania 9:11-14, Waebrania 10;10, Warumi 6:23, Warumi 5:8).
                                                                           

Ili uokolewe, sharti uweke imani yako juu ya kazi Yesu aliyoimaliza msalabani. Mtu akiamini kuwa Yesu alikufa mahali pa yeye ili amlipie gharama zake za dhambi na akafufuka tena basi mtu huyo ameokoka. Hakuna kitu mtu anachoweza kufanya mwenyewe binafsi ili aokoke. Hakun mwema wa kutosha kumpendeza Mungu kwa kuwa sote ni wenye dhambi (Isaya 64:6-7, Isaya 53:6). Lengine ni kwamba hakuna cha ziada maana kazi yote ilifanywa na kristo! Alipokuwa msalabani, Yesu alisema, “Imekwisha” (Yohana 19:30).

Kama vile haikugharimu chochote kuokolewa ila kuamini kazi iliyofanywa na Yesu msalabani vile vile hakuna kazi ambayo unahitajika kufanya ili upoteze wokovu wako. Kumbuka kazi ilifanywa na kumalizwa na yesu! Hakuna chochote kinachotegemea wewe mwenyewe katika wokovu. Yohana 10:27-29 inasema “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na ninawajua na wao hunifuata. Nami huwapa uzima wa milele; nao hawatapotea wala hakuna awezaye kuninyang’anya kutoka mikononi mwangu. Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa kutoka mikononi mwa Baba.”


Wengine hufikiria nakusema, “Nikiokolewa tu naweza kufanya kila nitakacho na wala sitapoteza wokovu wangu!” lakini wokovu si juu ya kuwa huru kufanya mapenzi yako. Wokovu ni kuwa huru kutoka kwa nyororo za dhambi ulizokuwa ukizitumikia iliuwe huru kumtumikia Mungu. Kadri waumini wanavyoishi duniani, kutakuweko na hali ya kupingana na dhambi katika miili yao. Kuishi na dhambi kunazuia ushirika na Mungu na muumini yeyote atakaye amua kuishi na dhambi hatafurahia ushirika wake na Mungu. Hata hivyo wakristo wanaweza kushinda dhambi kwa kulisoma na kulitumia neno la Mungu (biblia) maishani mwao na kuongozwa na Roho Mtakatifu – hiyo ina maana ya kujiachilia uongozwe na Roho katika kila shughuli ya siku na pia kupitia Roho uheshimu neno la Mungu.

Kwa hivyo, huku dini nyingine zikitaka waumini wao watende mambo Fulani Fulani au wasitende mambo Fulani ukristo ni juu ya kuwa na ushirika na Mungu. Deni lako la dhambi limelipwa na unaweza kuwa na ushirika na Mungu. Unaweza kuwa na ushindi juu ya maisha yako ya dhambi na ukatembea na ushirika na Mungu ukiwa mtiifu. Huwo ndiwo ukristo wa kweli unaoelezewa katika Biblia.