Tuesday, 9 September 2014

MUDA WA FARAGHA NA MUNGU

 Mtu, kwa hakika, ni jinsi alivyo peke yake faraghani na Mungu. Ili uwe kamili mwenyewe na kwa wengine, ni lazima uwe na muda wa kuwa na Mungu kila siku. Mojawapo ya yale tunayofundisha aliyeamini kwa mara ya kwanza ni kutenga wakati kila siku wa kuwa na Mungu, bila kubadilisha muda huo. Wanathiologia wa kale waliuita “Wakati wa Ukimya.” Nafikiri kwamba hayo maneno yanaeleza wakati huo vizuri. Je, una “Wakati wa Ukimya” kila siku? Kama sivyo, basi ni kwa nini? Ni vigumu sana kuwa mkristo katika umati wa watu kabla kuwa mkristo faraghani. Tabia yako mbele za watu huonyesha jinsi wakati wako na Mungu ulivyo. Ili kukua kiroho, kila muumini ni lazima ajenge maisha yake kwa muda wa faragha na Mungu.
 
Muda
Ni muda upi unaofaa kuwa na Mungu? Ikiwa wewe ni kama mfalme Daudi, basi kutana na Mungu kabla kuanza siku yako. Daudi alisema, “Asubuhi, Ewe Bwana waisikiliza sauti yangu; asubuhi naweka mahitaji yangu mbele yako…” Hili ni shauri nzuri. Bwana Yesu alikutana na Mungu kabla kuanza siku yake. “Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko” (Marko 1:35). Naona kwamba kama ilimbidi Yesu kuchukua muda kuwa na Baba yake kabla kukumbana na siku iliyojaa mambo mengi, mbona tusifanye hivyo? Sijali utafanya vipi, lakini fanya! Katika ratiba yako ya siku, weka wakati wa kuwa na Mungu katika nafasi ya kwanza.
 
Mahali
Yesu alienda mahali pa siri, kwa sababu alihitaji kuwa peke yake. Wewe pia wahitaji kufanya hivyo. Je, una mahali ambapo umetenga pa kusoma Bibilia yako na kuomba kila siku?
Je, ni mahali pa faragha ambapo unaweza kuomba kwa sauti bila kuwaamsha wengine? Ni kweli, maombi yana maana sana unapotenga wakati wa kuwa na Mungu. Masikio yako yanahitaji kusikia hisia za moyo wako. Kupaaza sauti kwa Mungu ni ishara ya mawasiliano kati ya mwenye dhambi na Baba yake aliyejawa na huruma. Je, unahitaji nini unapokutana na Mungu mahali ulipotenga? Unahitaji:
• Bibilia yako
• Daftari
• Kalamu
• Kitabu cha ibada (Devotional book)
• Kitabu cha kuandikia matukio ya kila siku (Journal for Daily accoutability)
Kujitoa
Itakubidi kuweka ahadi kati yako na Mungu kwamba utakutana naye kila asubuhi mahali fulani kwa muda fulani. Hebu fanya ahadi ya juma moja. Zingatia ahadi hiyo kwa kukutana naye. Labda utakuwa na wakati mzuri hata utamani kuendelea zaidi. Tahadhari! Shetani atakupinga. Atakuruhusu kwenda kanisani, kuimba katika kundi la waimbaji, na kufundisha katika darasa. Lakini shetani hutetemeka anapoona mtu mnyonge aliyetakaswa akiomba kwa magoti . Umtarajie kuleta mambo ya kuondoa mawazo yako kutoka kwa kuwa na muda wa faragha na Mungu! Anachukia na kuogopa muda wa faragha wa muumini kuwa na Mungu.
 
Taratibu
Baada ya kutenga nyakati za kukutana na Mungu, na kuwa na vifaa unavyohitaji, utafanayaje? Unaweza:
• Kuanza kwa maombi ya dakika nne
A=Adoration, ni kumsujudu Mungu. Anza kumsifu kwa nukta 60.
C=Confession, ni kutubu dhambi. Tubu kwa nukta 60.
T=Thanksgiving, ni kutoa shukurani. Msifu Bwana kwa baraka zako kwa nukta 60.
S=Supplication, ni kuombea wengine. Ombea wengine kwa nukta 60.
• Chagua somo katika maandiko.
Soma somo hilo kwa juma hilo lote. Anza na somo rahisi, kama vile Zaburi sura ya 1.
• Soma, chunguza, tafakari, na kutia katika akili.

Tumia daftari yako kuandika mawazo na maneno yenye maana. Mwombe Roho Mtakatifu akufunulie ukweli. Katika daftari yako, tenga sehemu ya maswahil kama vile: “Hii inamaanisha Mungu angependa nifanyeje?” Kufanya hivyo ni kuzingatia maandiko kibinafsi.
 
• Andika yale Baba anakuambia
Kila siku tumia daftari kuandika yale Mungu anakunenea kutoka kwa neno lake. Hii ni daftari yako ya siri ambayo itaonyesha kukua kwako, vita vyako, na ushindi unayopata. Kutokana nalo, labda utahitaji kuwazia wazo moja tu kila siku. Linaweza kuwa wazo kama vile, “leo nitaamini kwamba Yesu ananipenda kwa vyo vyote vile.”
 
• Zingatia wazo hilo.
Andika wazo hilo katika kijikaratasi na kulitazama mchana kutwa. Kufanya hivyo ni kutafakari maandiko.
 
• Tia akilini kifungu kimoja au vifungu viwili katika juma hilo. Zaburi 1 ni fupi sana, kwamba unaweza kuliweka akilini ukichagua kufanya hivyo.
 
• Funga wakati huo kwa maombi.
Jiombee, na uombe mwongozo wa Mungu kwa shughuli za siku hiyo. Omba maombi ya Yabesi,
inayopatikana katika 1 Mambo Ya Nyakati 4:9. Hii ni jinsi nzuri ya kuanza siku yako.

Ni mimi mpendwa wako:
Pastor Judicate F. Mnyone
Huduma: Glory of  Christ Tanzania Church (Ufufuo na Uzima) Dar-es-salaam
Simu: 0712545368
Barua Pepe: www.judicatemnyone@gmail.com



No comments:

Post a Comment