Wednesday, 8 June 2016

JINSI YA KUKUZA UHUSIANO WAKO NA ROHO MTAKATIFU (SEHEMU YA 1)

 
 
Na Mwl Judicate Fredy

Roho Mtakatifu yupo kwa watu wote wa mataifa walio
mwamini Bwana Yesu na kumpa maisha yao.
Nchini Marekali palitokea na mzee mmoja katika jimbo la Califonia ambaye alikuwa anaishi kwenye kachumba kadogo kalichojaa takataka, mzee huyu alikuwa akipita mitaani na kuokota takataka katika mapipa ya takataka kwa muda wa miaka kumi na watu wengi walimzoea, alikuwa ni mkimya sana asiyeongea na mtu lakini ilitokea siku hakuonekana kwa muda wa siku mbili na jirani yake alishangaa maana mzee yule alikuwa kila siku akibeba takataka kutokana katika pipa lake la takataka lakini kwa siku mbili hakumwona na takataka zilikuwa nyingi ndipo alipoenda kugonga kwake kwa muda mrefu bila majibu ndipo alipoamuwa kuingia ndani ya chumba chake na kukuta mwili wa mzee yule ukiwa sakafuni, polisi walipokuja waligundua mzee yule alikufa kwa njaa na baridi lakini cha kushangaza pembeni yake kulikuwa na sanduku ambalo alikuwa ameshikili na kufa likiwa mkononi ndipo polisi walipofungua na kukuta noti ya dola moja, saa aina ya Rolex ya dola 500 na box
la plastiki ambalo ndani yake kulikuwa na cheni za dhahabu na pete zenye almasi ambazo zen
ye thamani sawa na dola zaidi ya 22000, jambo hili liliweza kushangaza watu kuwa iliwezekana