Saturday, 14 May 2016

USHAURI NA MAOMBEZI

 
Wasiliana nami Mwl Judicate Fredy kwa:
 
Namba ya simu +255 765 544 589
             E-mail www.judicatemnyone@gmail.com
                                                      Facebook judicate_fredy

Natumaini kusikia kitu kwako, ukiwa na maswali juu ya kitu chochote kuhusu Neno la Mungu na maisha nitafute kwa mawasiliano hayo.

IJUE SIRI YA BOYFRIEND NA GIRLFRIEND 4

 
MAANA ILIYOFICHIKA YA GIRLFRIEND NA BOYFRIEND

Nataka ujue maana ya girlfriend na boyfriend, kama jinsi Shetani anavyoitumia, na jinsi anavyochochea tafsiri yake ndani ya watu wengi na kuwaangusha katika zinaa (dhambi)

Kwa maana ya ndani iliyofichwa na kufunikwa kwa maneno mazuri yaani girlfriend na boyfriend, ni hii; Ni uhusiano wakaribu sana kati ya watu wa jinsi tofauti na mara nyingi huambatana na kufanya ngono (zinaa)

Vijana wengi hawaukubali ukweli huu, na ndiyo maana nikakuuliza unapata hisia gani unaposema girlfriend au boyfriend wangu, tofauti na uposema rafiki yangu kwa hali ya kawaida? Kama na wewe unaipinga maana hiyo niliyokuambia fanya hivi; Jaribu kumuuliza msichana mwenye akili timamu kama anaye girlfriend, au muulize mvulana ambaye ni rafiki yako akuambie kama anaye boyfriend. Nina uhakika hatakupa jibu la moja kwa moja na ukipigwa usishangae, na usiseme Mwalimu Judicate amenituma.




"Mchumba ni mtu wa jinsia tofauti na wewe ambaye umemposa
 au umeposwa naye na tena umefanya naye shauri au
 patano au mkataba au agano kuwa utaoana naye".


    Vijana wengi hupenda kuwa na girlfriend au boyfriend wakiwa na maana ya urafiki wa kawaida, wakipendana, wakisaidiana na kushirikiana mambo mbalimbali mazuri.